Vitabu vya China vyavutia katika maonesho ya kimataifa ya vitabu nchini Algeria

(CRI Online) Novemba 13, 2024

Maonesho ya 27 ya Kimataifa ya Vitabu ya Algiers yanafanyika katika Kituo cha Maonyesho cha Pin Maritimes mjini Algiers, Algeria, ambapo vitabu vya China vimevutia wasomaji wenyeji wengi vijana wanaopenda kujua utamaduni na lugha ya Kichina.

Mwoneshaji vitabu kutoka China, Liu Ziwei amesema vitabu vingi vya China vinavyooneshwa ni kuhusu Pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, utamaduni na historia ya China, ujenzi wa mambo ya kisasa wa China pamoja na mafunzo ya lugha ya Kichina, ambavyo vimepokelewa vizuri na wasomaji wa Algeria.

Maonesho hayo yaliyoanza Novemba 6 na yamepangwa kumalizika Novemba 16, yanafanyika kwenye eneo lenye ukubwa wa mita za mraba elfu 23, yakishirikisha waonyeshaji 1,007 kutoka nchi 40 zikiwemo nchi saba za Afrika.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha