

Lugha Nyingine
Kenya yazindua mfumokazi wa kuboresha uchumi wa kazi za vibarua
Kenya imezindua mfumokazi mpya kwa ajili ya kuandaa dira ya kisera ili kuhimiza uchumi wake wa kazi za vibarua.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Kidigitali ya Kenya, Bibi Mary Kerema amesema mfumokazi huo wenye kichwa cha "mwongozo wa kisera kwa maendeleo ya uchumi wa kidijitali," unatoa dira jumuishi ya kuboresha uchumi wa ajira zisizo za kudumu nchini Kenya na kuunda sekta yenye usawa na endelevu zaidi kwa wafanyakazi zaidi ya milioni moja na biashara zinazotokana na kazi hizo.
“Mfumokazi huo unatoa sera ya kina kama mwongozo wa kukuza uchumi wa kidijitali nchini Kenya” amesema Bibi Kerema kwenye hafla ya uzinduzi wa mfumokazi huo.
Amebainisha kuwa mfumokazi huo utaanzisha mikakati mipya inayolenga kupanua ufikiaji wa huduma za kidijitali na kuhimiza ukuaji endelevu wa uchumi wa kidijitali.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma