China kuongeza mshikamano, ushirikiano na nchi za Latini Amerika: msemaji wizara ya mambo ya nje

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 14, 2024

BEIJING - China itaendelea kuongeza mshikamano na ushirikiano na nchi za Latini Amerika, na kutoa hali nzuri zaidi ya kuridhika na furaha kwa watu wa pande zote mbili, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Lin Jian amesema Jumatano.

Akizungumza kuhusu midoli ya alpaca va Peru, "warmpaca," kuwa moja ya bidhaa moto moto kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE) ya mwaka huu, msemaji Lin amesema kwamba fundi wa Sanaa za mikono wa Peru, Oswaldo Mamani ambaye awali alikuwa na karakana ya ghorofa moja kwenye jengo la maghorofa mengi na mauzo ya kila mwaka ya vitu zaidi ya 100, lakini sasa karakana yake inachukua ghorofa tatu huku mamia ya mafundi wa kazi za mikono wakijiunga naye.

Mamani alisema katika mahojiano kuwa China ni neema kwake na kwa wanakijiji wenzake kwa sababu nchi hiyo imewawezesha kupata mapato zaidi na kuishi maisha bora zaidi.

"China na Latini Amerika kwa muda wote zimeipa kipaumbele miradi mikuu ya shughuli za maisha ya watu katika ushirikiano wao. Orodha ya simulizi za kuinua maisha na kugusa moyo kama vile 'warmpaca' inaendelea," Lin amesema.

Mradi wa usambazaji umeme wa Belo Monte UHV, ambao unaunda "njia ya haraka ya umeme" inayounganisha kaskazini na kusini mwa Brazili, si tu umetoa nishati ya kutosha kwa vituo vya viwanda huko, lakini pia umetatua tatizo la uhaba wa umeme kwa Wabrazili zaidi ya milioni 22, Lin amesema.

China pia imetekeleza idadi kubwa ya miradi midogo midogo na yenye kupendeza ya maisha ya watu katika Latini Amerika, kama vile miradi ya msaada wa China ya usambazaji maji katika miji miwili ya Costa Rica ambayo imenufaisha wenyeji na uchumi pia, ameongeza.

"China itafuata kanuni ya udhati, matokeo halisi, upendo na nia njema na kanuni ya kutafuta maslahi makubwa zaidi na ya pamoja, kujikita katika maisha ya watu, ambacho ni kipaumbele katika uhusiano wake na Latini Amerika, kuendelea kuongeza mshikamano na ushirikiano na nchi za Latini Amerika, na kutoa hali nzuri zaidi ya kuridhika na furaha kwa watu wa pande zote mbili," Lin amesema.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha