

Lugha Nyingine
Mkutano wa kwanza wa “Jukwaa la Wudadao” wafanyika kwa mafanikio mjini Tianjin, China
Mkutano wa kwanza wa “Jukwaa la Wudadao” la Tianjin lenye mada kuu ya "Ujenzi wa Mambo ya Kisasa wa mtindo wa China na Njia Kuu Duniani " limefanyika kwa mafanikio katika Jumba la Qingwangfu mjini Tianjin, tarehe 12 Novemba, 2024.
Mkutano huo wa Jukwaa hilo unalenga kusoma zaidi, kueneza na kutekeleza kwa kina misingi ya Mkutano wa Tatu wa Wajumbe Wote wa Kamati Kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na hotuba muhimu ya Katibu Mkuu Xi Jinping wa kamati kuu ya chama wakati wa ziara yake ya ukaguzi katika Mji wa Tianjin, kutekeleza fikra ya Xi Jinping kuhusu mambo ya kidiplomasia, na kuongeza zaidi uzoefu wa Tianjin wa kutekeleza Pendekezo la Ustaarabu wa Dunia.
Wataalamu na wasomi wengi kutoka vyuo vikuu maarufu na jumuiya za washauri bingwa za China wamebadilishana mawazo na kufanya majadiliano ya kina juu ya mada za "Dhana Mpya za Maendeleo na Ujenzi wa Mambo ya Kisasa wa China", "Pendekezo la Ustaarabu wa Dunia na Ujenzi wa Jumuiya ya Binadamu yenye Mustakabali wa Pamoja", na "Ufunguaji Mlango wa Kiwango cha Juu na Kujenga 'Tianjin ya Duniani '".
Katika ufunguzi wa mkutano wa jukwaa hilo, ilianzisha Kamati ya Wataalamu Washauri wa Maendeleo ya Kimataifa ya Mji wa Tianjin, ikilenga kukusanya hekima kutoka pande zote, kufanya juhudi zaidi za kujenzga Tianjin kuwa mji wa maendeleo ya kimataifa, kuharakisha ujenzi wa mji wa mambo ya kisasa wa kijamaa wa Tianjin, na kuhimiza kihalisi ujenzi wa mambo ya kisasa wa mtindo wa China kwa kupitia ujenzi wa miji ya maendeleo ya kimataifa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma