

Lugha Nyingine
Hezbollah yasema makao makuu ya wizara ya ulinzi ya Israel kushambuliwa kwa mara ya kwanza
Helikopta ya kijeshi ya Israeli ikitekeleza jukumu katika operesheni ya kijeshi karibu na mpaka wa kaskazini wa Israel na Lebanon, Novemba 13, 2024. (Picha na Gil Cohen Magen/Xinhua)
BEIRUT - Hezbollah imesema Jumatano alasiri kwamba, tokea mgogoro uanze sasa kati yake na Israeli, kwa mara ya kwanza imelenga mashambulizi dhidi ya makao makuu ya wizara ya ulinzi ya Israeli.
Imesema katika taarifa yake kwamba ilianzisha shambulizi la kupiga mabomu kutoka angani dhidi ya kituo cha Kirya cha makao makuu ya wizara ya ulinzi ya Israeli huko Tel Aviv, shambulizi hilo lilifanywa na kikosi chake cha droni za kujitolea mhanga.
Imesema kuwa shambulizi hilo limefanywa ili kuunga mkono watu wa Palestina huko Gaza, na kuilinda Lebanon na watu wake.
Jeshi la Israel bado halijatoa maelezo yoyote kuhusu shambulizi hilo.
Tangu Septemba 23, Jeshi la Israel limekuwa likizidisha mashambulizi yake ya kupiga mabomu kutoka angani dhidi ya Lebanon, na mgogoro kati yake na Hezbollah umepamba moto. Mwanzoni mwa mwezi Oktoba, Israel ilianzisha zaidi operesheni ya ardhini kuvuka mpaka wake wa kaskazini na kuingia Lebanon.
Wizara ya afya ya Lebanon ilisema kuwa, kutokana na mashambulizi hayo ya Israeli ya kupiga mabomu kutoka angani tangu mgogoro ulipoanza mwezi Oktoba mwaka jana, idadi ya watu waliofariki dunia imefikia 3,287, huku majeruhi wakifikia 14,222.
Ndege ya kivita ya Israeli ikiruka kuelekea Lebanon katika operesheni ya kijeshi, kama ilivyoonekana kutoka mpaka wa kaskazini wa Israel na Lebanon, Novemba 13, 2024. (Picha na Gil Cohen Magen/Xinhua)
Ndege ya kivita ya Israeli ikiruka kuelekea Lebanon katika operesheni ya kijeshi, kama ilivyoonekana kutoka mpaka wa kaskazini wa Israel na Lebanon, Novemba 13, 2024. (Picha na Gil Cohen Magen/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma