

Lugha Nyingine
Umoja wa Mataifa waanzisha mradi wa kupinga mirengo ya itikadi kali za vurugu katika nchi za Afrika Mashariki
Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) jana Jumatano limeanzisha mradi wa kujenga amani na kupinga mirengo yenye itikadi kali za vurugu kwa ajili ya nchi za Afrika Mashariki.
Mwakilishi mkazi wa shirika hilo nchini Kenya Anthony Ngororano amesema kuwa mradi huo uliotengewa bajeti ya dola za kimarekani milioni 18 unalenga kujenga ustahimilivu wa jamii katika nchi za Kenya, Somalia na Sudan Kusini.
Amesema, jamii zitakazofaidika na mradi huo zitapokea simulizi na ujumbe wa kupinga kauli za chuki, habari potofu na itikadi kali zinazohimiza matendo ya vurugu kupitia elimu ya amani katika vyombo vya habari na mazungumzo ya kijamii.
Pia ameongeza kuwa mradi huo wa miaka mitatu unatarajiwa kuimarisha utayari na mwitikio wa jamii kupitia kuboresha taratibu za tahadhari ya mapema ili kukabiliana na mirengo ya itikadi kali za vurugu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma