

Lugha Nyingine
Maofisa wa Afrika wahimiza uwekezaji katika gridi ndogo ili kushughulikia umaskini wa nishati
NAIROBI - Uwekezaji endelevu katika gridi ndogo ni muhimu katika kupanua ufikiaji wa nishati safi kwa jamii ambazo hazijaunganishwa kwenye gridi za taifa za umeme barani Afrika, maafisa wamesema kwenye kongamano la mtandaoni siku Jumatano.
John Ouko, afisa mkuu wa uendeshaji katika Jumuiya ya Waendelezaji wa Gridi Ndogo ya Afrika, ambayo ni jumuiya ya wazengezi wa sekta ya umeme, amesema bara hilo linapaswa kuchunguza miundo vumbuzi ya ufadhili wa kutekeleza miradi ya kijamii ambayo inatoa matumanini ya upatikanaji wa umeme wa bei nafuu, uhakika na safi zaidi.
"Gridi ndogo zinapaswa kuchukuliwa kuwa njia ya gharama nafuu zaidi ya kufikia upatikanaji wa nishati kwa wote barani Afrika huku zikitoa suluhu kwa janga la tabianchi," Ouko amesema kwenye kongamano hilo la mtandaoni, lenye mada yenye kichwa cha "Kufadhili gridi ndogo za nishati mbadala barani Afrika," akiongeza kuwa mifuko ya pensheni na mikopo midogo midogo itumike kikamilifu ili kuanzisha miradi midogo ya umeme katika maeneo ya pembezoni ya bara hilo.
Kwa mujibu wa Ouko, nchi za Afrika zinapaswa kushughulikia mapengo ya ufadhili, kiufundi, na udhibiti ambayo yamedhoofisha maendeleo makubwa ya gridi ndogo, hali ambayo imeathiri vibaya maendeleo ya vijijini na hatua za tabianchi.
Amesema kuwa kampuni zinazojenga gridi ndogo katika bara hilo zinahitaji madeni ya muda mrefu na ya gharama nafuu, kanuni rafiki, na kutoa mafunzo mapya kwa wafanyakazi wao ili kuanzisha mifumo ya nishati safi inayostahimili.
Joshua Amponsem, mwanzilishi wa Shirika la Kijani la Vijana la Afrika, ambalo ni shirika la uzengezi wa uendelevu wa mazingira lenye makao yake nchini Ghana, amesema kuwa zote sekta ya umma na ya kibinafsi zinapaswa kufungua mtaji kuelekea maendeleo ya gridi ndogo na kusaidia kuunganisha watu milioni 600 barani Afrika ambao wanakosa huduma ya umeme.
Amponsema amekiri uwezo mkubwa wa Afrika katika sekta ya nishati mbadala, zikiwemo umeme wa nishati ya maji, ya nishati ya jua, na ya upepo ambao unapaswa kutumiwa ili kuweka gridi ndogo katika maeneo ya vijijini kusaidia kilimo cha umwagiliaji, usindikaji wa mazao ya kilimo na viwanda vyepesi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma