Taasisi za Kifedha za kigeni zinakaribishwa kuwekeza nchini China: Naibu Waziri Mkuu wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 15, 2024

Naibu Waziri Mkuu wa China He Lifeng, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akikutana na Mwenyekiti wa Kundi la HSBC Mark Tucker mjini Beijing, mji mkuu wa China, Novemba 14, 2024. (Xinhua/Pang Xinglei)

BEIJING - China inakaribisha taasisi zaidi za kifedha na mtaji wa muda mrefu wa kigeni kuwekeza na kufanya shughuli zao nchini China, Naibu Waziri Mkuu wa China, He Lifeng ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) amesema mjini Beijing siku ya Alhamisi alipokutana na Mwenyekiti wa Kundi la HSBC, Mark Tucker.

He Lifeng amesema, China inafanya juhudi za kuzidisha mageuzi ya mfumo wake wa kifedha, kupanua ufunguaji mlango wa kitaasisi katika sekta yake ya mambo ya fedha hatua kwa hatua, na kuweka mazingira ya kitaasisi yenye uwazi, thabiti na yanayotabirika, yakitoa urahisi zaidi kwa kampuni za kigeni kupanua biashara zao nchini China.

Tucker amesema kuwa Kundi la HSBC lina imani na matarajio juu ya uchumi na soko la kifedha la China, na litaendelea kupanua uwekezaji wake nchini China.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha