China na Russia kuendeleza ushirikiano wa utekelezaji sheria na usalama

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 15, 2024

Chen Wenqing, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni Katibu wa Kamati ya Masuala ya Kisiasa na Kisheria ya Kamati Kuu ya CPC, akipeana mkono na Sergei Shoigu, Katibu wa Baraza la Usalama la Russia, kabla ya kuongoza kwa pamoja mkutano wa 9 wa mfumokazi wa ushirikiano wa utekelezaji sheria na usalama kati ya China na Russia mjini Beijing, mji mkuu wa China, Novemba 13, 2024. (Xinhua/Li Xiang)

BEIJING - Mkutano wa 9 wa mfumokazi wa ushirikiano wa utekelezaji sheria na usalama kati ya China na Russia umefanyika Beijing siku ya Jumatano ambapo Chen Wenqing, aliongoza mkutano huo pamoja na Sergei Shoigu Katibu wa Baraza la Usalama la Russia.

Chen, mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC na Katibu wa Kamati ya Masuala ya Kisiasa na Kisheria ya Kamati Kuu ya CPC, amesema katika miaka ya hivi karibuni wakuu wa nchi hizo mbili wamefikia makubaliano kadhaa muhimu katika kuendeleza Ushirikiano wa Kimkakati wa Pande Zote wa Uratibu kwa Zama Mpya kati ya China na Russia, huku uhusiano wa pande mbili ukiendelezwa kwa ngazi ya juu.

Akisema kuwa mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Russia, Chen amesema China inapenda kufanya kazi na Russia ili kutekeleza kikamilifu makubaliano muhimu yaliyofikiwa na wakuu wa nchi hizo mbili na kusukuma mbele kwa ajili ya maendeleo tulivu na ya muda mrefu ya uhusiano kati ya China na Russia katika zama mpya.

Tangu kuanzishwa kwa mfumokazi wa ushirikiano wa utekelezaji sheria na usalama kati ya China na Russia miaka 11 iliyopita, idara husika za nchi hizo mbili zimeshirikiana kwa karibu katika kulinda usalama wa siasa, mapambano dhidi ya ugaidi na msaada wa utekelezaji wa sheria, na kupata matokeo mengi ya halisi.

China ina nia ya kuzidisha mawasiliano ya kimkakati na Russia, kuhimiza uratibu na ushirikiano wa karibu kati ya idara za pande hizo mbili, kufanya kazi pamoja zaidi katika kulinda usalama wa siasa, usalama wa mtandaoni, usalama wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” na kupambana na uhalifu wa kuvuka mipaka, ili kuhakikisha maendeleo na utulivu wa jumla wa nchi hizo mbili, Chen ameongeza.

Kwa upande wake Shoigu amesema Russia inapenda kuendeleza kikamilifu ushirikiano katika mambo ya usalama na utekelezaji wa sheria na China ili kulinda vyema zaidi maslahi ya usalama ya nchi zote mbili.

Chen Wenqing, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni Katibu wa Kamati ya Masuala ya Kisiasa na Kisheria ya Kamati Kuu ya CPC, akiongoza kwa pamoja mkutano wa 9 wa mfumokazi wa ushirikiano wa utekelezaji sheria na usalama kati ya China na Russia na Sergei Shoigu, Katibu wa Baraza la Usalama la Shirikisho la Russia, mjini Beijing, mji mkuu wa China, Novemba 13, 2024. (Xinhua/Li Xiang)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha