Biashara ya bidhaa kati ya China na LAC inatarajiwa kuendelea kukua kwa kasi kubwa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 15, 2024

BEIJING - Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Lin Jian amesema Alhamisi kuwa, China inaamini biashara ya bidhaa kati ya China na nchi za Latini Amerika na Caribbean (LAC) itaendelea kukua kwa kasi ya juu na kupata matokeo yenye manufaa kwa pande zote kwenye kiwango cha juu zaidi.

Lin alisema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari alipotoa maoni yake kuhusu ushirikiano wa kibiashara na kiuchumi kati ya China na Latini Amerika na Caribbean.

Ripoti iliyotolewa hivi karibuni na Kamisheni ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa kwa Eneo la Latini Amerika na Caribbean (ECLAC) ilisema kuwa, China ni mshirika muhimu wa biashara na soko la mauzo ya nje linalokua kwa kasi zaidi kwa Latini Amerika na Caribbean.

Kufanya ushirikiano wa kunufaishana na kutafuta maendeleo kwa pamoja ni kanuni kuu ya ukuaji wa uhusiano kati ya China na eneo hilo, Lin amesema, akieleza kuwa katika robo tatu za kwanza za mwaka huu, thamani ya biashara kati ya pande hizo mbili ilifikia dola za Marekani bilioni 427.4, na kupata ongezeko la asilimia 7.7 kuliko mwaka uliopita, na thamani ya jumla ya biashara ya mwaka mzima inatarajiwa kuzidi dola bilioni 500 za Marekani.

Lin ameendelea kusema kuwa tangu mwanzoni mwa karne mpya, biashara ya bidhaa kati ya China na Latini Amerika na Caribbean imekua kwa kasi zaidi kuliko ile ya dunia, huu ni msingi wa kuweza kusaidiana zaidi kati ya nchi hizo mbili katika sekta ya uchumi.

Ameeleza kuwa Chile imekuwa chanzo cha pili kwa ukubwa wa uagizaji matunda freshi wa China kutoka nje, na mnyororo wa viwanda vya nishati mpya wa China unatoa mpango wa kuleta faida kubwa zaidi kwa ajili ya kubadilisha muunndo wa uzalishaji kuwa wa kijani katika eneo hilo.

Kuongezeka kwa biashara ya bidhaa kati ya China na Latini Amerika na Caribbean kunaungwa mkono na soko kubwa na matarajio mazuri kati ya pande hizo mbili, amesema Lin.

"Kwa vile China na Latini Amerika na Caribbean kila upande unachukulia upande mwingine ni fursa yake ya kupata maendeleo, China inaamini kuwa kwa juhudi za pande zote mbili, biashara ya bidhaa itaendelea kukua kwa kasi kubwa na kufikia matokeo yenye manufaa kwa pande zote kwenye kiwango cha juu zaidi." amesema Lin. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha