China yaahidi kufanya vitendo halisi vya kuhimiza mshikamano na ushirikiano wa Asia na Pasifiki

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 18, 2024

Rais Xi Jinping wa China akitoa hotuba muhimu isemayo "Kubeba Wajibu wa Nyakati Zetu na Kuhimiza kwa Pamoja Maendeleo ya Asia na Pasifiki" kwenye Mkutano wa 31 wa Viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya APEC uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha  Lima cha Peru, Novemba 16, 2024. (Xinhua/Xie Huanchi)

LIMA - Rais wa China Xi Jinping ametangaza Jumamosi kuwa China itakuwa mwenyeji wa mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia Pasifiki (APEC) Mwaka 2026, na inapenda kushirikiana na pande zote ili kuzidisha ushirikiano wa Asia na Pasifiki.

Amesema hayo alipokuwa akihutubia Mkutano wa 31 wa Viongozi wa Jumuiya ya APEC uliofanyika katika mji mkuu wa Peru. Chini ya kaulimbiu ya mwaka huu ya “Wezesha, Jumuisha, Kua", nchi wanachama wa APEC zimekubali kufanya juhudi za kujenga jumuiya ya Asia na Pasifiki iliyo ya ufunguaji mlango, yenye uhai, himilivu na amani katika wakati wa kukabiliwa na changamoto na hali nyingi zisizokuwa na uhakika.

Wafanyakazi wakiwa wamekusanyika karibu na bango katika eneo la mkutano wa G20  huko Rio de Janeiro, Brazili, Novemba 16, 2024. (Xinhua/Wang Tiancong)

Wafanyakazi wakiwa wamekusanyika karibu na bango katika eneo la mkutano wa G20 huko Rio de Janeiro, Brazili, Novemba 16, 2024. (Xinhua/Wang Tiancong)

Mawasiliano ya karibu na APEC

Ili kuendeleza ushirikiano wa Asia na Pasifiki, China imefanya jitihada ya kubeba jukumu hilo kwa kujitolea kuwa mwenyeji wa mkutano wa APEC wa Mwaka 2026, imekaribishwa na nchi wanachama wa APEC na kupata uungaji mkono wao kwenye Mkutano wa Viongozi wa Jumuiya ya APEC wa mwaka huu, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China alisema Jumamosi.

"Tunatarajia kushirikiana na pande zote ili kuimarisha ushirikiano wa Asia na Pasifiki na kuleta manufaa kwa watu wa eneo hilo," Rais Xi amesema kwenye hotuba yake.

Rais Xi Jinping wa China akitoa hotuba muhimu isemayo "Kubeba Wajibu wa Nyakati Zetu na Kuhimiza kwa Pamoja Maendeleo ya Asia na Pasifiki" kwenye Mkutano wa 31 wa Viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya APEC uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Lima cha Peru, Novemba 16, 2024. (Xinhua/Xie Huanchi)

Rais Xi Jinping wa China akitoa hotuba muhimu isemayo "Kubeba Wajibu wa Nyakati Zetu na Kuhimiza kwa Pamoja Maendeleo ya Asia na Pasifiki" kwenye Mkutano wa 31 wa Viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya APEC uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Lima cha Peru, Novemba 16, 2024. (Xinhua/Xie Huanchi)

Wito wa maendeleo bora ya Asia na Pasifiki

Kwenye hotuba yake hiyo, Rais Xi ametoa wito kwa nchi za APEC "kuwa na mshikamano na ushirikiano ili kukabiliana na changamoto, kutimiza kwa pande zote Matarajio ya Putrajaya ya Mwaka 2040, kujenga jumuiya ya Asia na Pasifiki yenye mustakabali wa pamoja, na kuanza zama mpya za maendeleo ya Asia na Pasifiki. "

"Tunapaswa kushikilia ushirikiano wa pande nyingi na uchumi ulio wa ufunguaji mlango, kulinda kithabiti mfumo wa biashara ya pande nyingi chini ya kiini chake cha Shirika la Biashara Duniani, kuchochoea kikamilifu umuhimu wa APEC kama kitotoleo cha kanuni za uchumi na biashara duniani, na utandawazi wa kiuchumi wa kikanda na mafungamano ya mawasiliano yake," amesema Rais Xi.

Rais wa China Xi Jinping na viongozi na wawakilishi wengine kutoka nchi wanachama wa APEC  wakipiga picha pamoja  huko Lima, Peru, Novemba 16, 2024. (Xinhua/Huang Jingwen)

Rais wa China Xi Jinping na viongozi na wawakilishi wengine kutoka nchi wanachama wa APEC wakipiga picha pamoja huko Lima, Peru, Novemba 16, 2024. (Xinhua/Huang Jingwen)

Dhamira ya mustakabali wa pamoja

Ufunguaji mlango ni alama wazi ya ujenzi wa mambo ya kisasa wa China, na siku zote China inajikita katika kupiga hatua kubwa ya kufungua mlango wake kwa dunia.

China inaendelea kufuata kigezo cha juu katika kutekeleza “Makubaliano ya Uhusiano wa Wenzi wa Kiuchumi wa Kikanda” , na pia inafanya juhudi za kuhimiza kujiunga na “Makubaliano ya Wenzi wa Pande zote na Maendeleo ya Kuvuka-Pasifiki na “Makubaliano ya Uhusiano wa Wenzi wa Uchumi wa Kidijitali”, Rais Xi amesema.

"China inakaribisha pande zote kuendelea kupanda 'treni ya mwendokasi' ya maendeleo yake na kukua pamoja na uchumi wa China ili kutoa mchango kwa ajili ya ujenzi wa mambo ya kisasa wa nchi zote katika maendeleo ya amani, ushirikiano wa kunufaishana na ustawi wa pamoja," ameongeza.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha