Biashara kati ya China na Brazil yakua kwa asilimia 9.9 katika miezi 10 ya kwanza ya 2024

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 18, 2024
Biashara kati ya China na Brazil yakua kwa asilimia 9.9 katika miezi 10 ya kwanza ya 2024
Picha iliyopigwa Machi 12, 2024 ikionyesha kiwanda cha betri cha BYD mjini Manaus, mji mkuu wa Jimbo la Amazonas, Brazili. (Xinhua/Wang Tiancong)

BEIJING - Biashara kati ya China na Brazil imeongezeka kwa asilimia 9.9 katika kipindi cha miezi 10 ya kwanza ya Mwaka 2024 kuliko kipindi kama hicho mwaka jana, ikionyesha kuimarika kwa uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya nchi hizo mbili.

Kiwango hicho cha ukuaji kilikuwa asilimia 4.7 zaidi ya kiwango cha ukuaji wa jumla wa biashara ya nje ya China, kama inavyoonyeshwa kwenye takwimu za Mamlaka Kuu ya Forodha ya China zilizotolewa jana Jumapili.

Biashara kati ya China na Brazili ilifikia yuan trilioni 1.14 (dola za kimarekani bilioni 158.33) kuanzia Januari hadi Oktoba, ikiwemo yuan bilioni 432.08 katika mauzo ya nje na yuan bilioni 708.15 katika uagizaji nje bidhaa, zote zikidumisha ukuaji tulivu.

Mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Brazil. Katika miaka 50 iliyopita,nchi hizo mbili zimepata mafanikio yenye matunda katika ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara na maendeleo makubwa katika uhusiano wa pande mbili wa kiuchumi na kibiashara.

China imekuwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara na chanzo cha mauzo ya nje ya Brazili kwa miaka 15 mfululizo iliyopita, huku Brazili kwa muda mrefu imekuwa mshirika mkuu wa kibiashara wa China katika Latini Amerika.

Kutokana na kuongezeka kwa ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara, bidhaa bora zaidi kutoka Brazil zinaingia kwenye soko la China. Katika miezi 10 ya kwanza ya mwaka huu, sehemu ya China katika mauzo ya nje ya Brazili ya soya na madini ya chuma ilizidi asilimia 70, na sehemu ya China katika mauzo ya nje ya rojo na mafuta ghafi ilizidi asilimia 40.

Bidhaa bora zaidi za viwanda kutoka China zinaingia Brazili. China iliuza bidhaa za kati zenye thamani ya Yuan bilioni 216.86 kwa Brazili katika miezi 10 ya kwanza, ongezeko la asilimia 11.8 mwaka hadi mwaka, ikichukua nusu ya thamani ya jumla ya mauzo ya nje ya China kwenda Brazili.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha