Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China asema ombi la China kuwa mwenyeji wa mkutano wa APEC mwaka 2026 limeungwa mkono na pande zote

(CRI Online) Novemba 18, 2024

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China amesema ombi la China kuwa mwenyeji wa mkutano wa kilele wa APEC mwaka 2026 limeungwa mkono na pande zote husika na kuidhinishwa katika mkutano wa viongozi wa APEC uliomalizika mwishoni mwa wiki.

Akijibu swali la mwandishi wa habari kuhusu suala husika kwenye mkutano na waandishi wa habari, msemaji huyo ameeleza kuwa APEC ni mfumo muhimu wa ushirikiano wa kiuchumi katika eneo la Asia-Pasifiki na kwa kuzingatia hali ya jumla ya kukuza ushirikiano wa Asia-Pasifiki, China imejitolea kubeba majukumu yake na kutoa ombi la kuwa mwenyeji wa mkutano wa APEC wa 2026, ambalo limekaribishwa na nchi wanachama wa APEC na limeidhinishwa na mkutano wa viongozi wa APEC wa mwaka huu.

“China siku zote imekuwa ikiweka umuhimu mkubwa katika ushirikiano wa Asia-Pasifiki na iliwahi kuwa mwenyeji wa mikutano ya APEC ya mwaka 2001 na 2014. Mwaka 2026, itakuwa mara ya tatu kwa China kuandaa mkutano wa APEC” msemaji huyo amesema.

Amesema, China inapenda kuimarisha mawasiliano na ushirikiano na pande zote katika maandalizi ya mkutano huo wa mwaka 2026, kutekeleza kwa pamoja Dira ya 2040 ya Putrajaya, kuhimiza ujenzi wa Jumuiya ya Asia-Pasifiki na eneo la Biashara Huria la Asia-Pasifiki, kuhimiza matokeo halisi ya ushirikiano katika sekta mbalimbali, na kutoa msukumo mpya kwa ukuaji wa uchumi wa Asia-Pasifiki na dunia kwa ujumla.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha