Lugha Nyingine
Mradi wa Bustani ya Jiolojia ya Ngorongoro Lengai unaofadhiliwa na China waanzishwa rasmi nchini Tanzania
(Picha inatoka wechat ya Xinhua)
Ujenzi wa mradi wa bustani ya Jiolojia Ngorongoro Lengai unaofadhiliwa na China katika mkoa wa Arusha, kaskazini mwa Tanzania, umeanzishwa rasmi Jumamosi kwa kuweka jiwe la msingi.
Agnes Gidna, meneja wa mradi wa Jumba la makumbusho la bustani hiyo, alisema kuwa lengo la mradi huo ni kulinda, kuhifadhi, na kuendeleza urithi wa kijiolojia na kitamaduni wa eneo hilo, wakati inapokuza utalii endelevu.
Waziri wa Maliasili na Utalii wa Tanzania, Pindi Chana aliishukuru serikali ya China kwa msaada wake, akisema kuwa mradi huo siyo tu unaboresha uzoefu wa wageni bali pia utaifanya Tanzania kuwa mojawapo ya maeneo bora ya utalii duniani.
“Mradi huu utainua hadhi ya Tanzania dunaini katika utalii, uhifadhi na urithi wa kitamaduni,” Chana alisema.
Balozi wa China nchini Tanzania, Chen Mingjian, alisema kuwa mradi huu ni mpango wa kwanza wa msaada wa bustani ya jiolojia wa China nje ya nchi, uliosainiwa na viongozi wa nchi hizo mbili mjini Beijing.
“Mara baada ya kukamilika, mradi huu siyo tu itaboresha uhifadhi na usimamizi wa bustani ya Jiolojia ya Ngorongoro-Lengai bali pia utaimarisha utafiti wa jiolojia na sekta ya utalii nchini Tanzania," alisema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma