Lugha Nyingine
Rais wa Kenya asema diplomasia ya kiuchumi inasalia kuwa msingi wa sera mpya ya mambo ya nje
Rais wa Kenya William Ruto amesema serikali yake imepitia sera yake ya mambo ya nje ili kuifanya iitikie zaidi mahitaji ya raia, na mwelekeo unaotokea wa kimataifa, huku diplomasia ya uchumi ikiendelea kuwa msingi wa mawasiliano ya kimataifa ya nchi hiyo.
Akiongea kwenye mkutano wa mashauriano uliofanyika Nairobi, Kenya, Ruto alisema sera mpya ya mambo ya nje, ambayo imetayarishwa, inazingatia watu na itasaidia nchi kuvutia uwekezaji na kupata nafasi yake sahihi katika jukwaa la kimataifa.
Alisema kuwa sera hiyo itahakikisha mawasiliano ya kidiplomasia ya Kenya yanaleta manufaa yanayoonekana kwa kila Mkenya na kufungua nguvu ya ushirikiano. Aidha alisisitiza kuwa Kenya itainua nafasi yake kama kituo cha mambo ya fedha cha kikanda, ikiungwa mkono na sekta thabiti ya benki na kuwa mwenyeji wa kituo kikubwa zaidi cha Benki ya Dunia nje ya Washington, ili kuendesha diplomasia yake ya kiuchumi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma