Lugha Nyingine
Rwanda yaadhimisha siku ya watoto duniani na kutoa wito wa kukomesha unyanyasaji wa kifamilia
Rwanda imeungana na jumuiya ya kimataifa katika kuadhimisha Siku ya Watoto Duniani, ikiwa na wito wa kukomesha unyanyasaji wa kifamilia unaoendelea kutishia haki za watoto.
Kwenye sherehe hizo zilizofanyika mjini Kigali, mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Mtoto la Rwanda (NCDA) Assumpta Ingabire amesema kuwa kulea watoto ni jukumu lisiloweza kubadilishwa. Ili kuhakikisha ukuaji na maendeleo yao mazuri, lazima watengenezewe mazingira yatakayowawezesha kustawi na kukua na kuwa raia wema. Lazima ukomeshwe unyanyasaji wa kifamilia.
Amesisitiza matatizo makubwa yanayoathiri watoto, ikiwa ni pamoja na kudumaa kwa watoto na unyanyasaji wa nyumbani, ambao mara nyingi yanawalazimisha watoto kuingia mitaani. Pia amesisitiza umuhimu wa kulea watoto kwa kuwajibika katika kutatua changamoto hizo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma