Zimbabwe kuinua uhusiano wake na China ili kuharakisha ukuaji wa viwanda

(CRI Online) Novemba 21, 2024

Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara ya Kimataifa wa Zimbabwe Amon Murwira alisema Jumatano kuwa azma ya Zimbabwe ya kubadilika na kuwa nchi yenye uchumi wa mapato ya kati unaoendeshwa kwa maarifa na viwanda vingi ifikapo mwaka 2030 inaweza kufikiwa kwa kuimarisha uhusiano kati yake na China.

Hayo yamo kwenye hotuba iliyosomwa kwa niaba yake katika Kongamano la Biashara kati ya Zimbabwe na China lililofanyika Harare, Zimbabwe, ambapo amesema kuwa mabadiliko hayo yatawezekana kama wataongeza ushirikiano wao wa kiuchumi na China ambayo ni mshirika wao wa kimkakati kwa faida ya jamii na uchumi wa pande mbili, ambapo watu wataishi maisha yenye ustawi, ufanisi na ya kuridhisha.

Murwira alisema kongamano la mwaka huu linakuja wakati biashara kati ya China na Zimbabwe imepata ukuaji mkubwa, na pia imepata msukumo mkubwa kufuatia kusainiwa kwa makubaliano ya biashara kati ya nchi hizo mbili wakati wa Mkutano wa Kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika mwezi Septemba.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha