Mkutano wa Kilele wa Wuzhen wa Baraza la Mtandao wa Intaneti la Dunia wasisitiza siku za baadaye za kidijitali za kutilia maanani maslahi ya binadamu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 22, 2024

Tarehe 20, Novemba, 2024, mkutano wa kilele wa Wuzhen wa Baraza la Mtandao wa Intaneti la Dunia 2024 ulifunguliwa huko Wuzhen, Mkoa wa Zhejiang wa China. (Xinhua/Huang Zongzhi)

Tarehe 20, Novemba, 2024, mkutano wa kilele wa Wuzhen wa Baraza la Mtandao wa Intaneti la Dunia 2024 ulifunguliwa huko Wuzhen, Mkoa wa Zhejiang wa China. (Xinhua/Huang Zongzhi)

Mkutano wa kilele wa Wuzhen wa Baraza la Mtandao wa Intaneti la Dunia 2024 ulifunguliwa asubuhi ya tarehe 20 huko Wuzhen, Mkoa wa Zhejiang wa China. Mkutano huo umesisitiza kujenga siku za baadaye za kidijitali zilizo za kutilia maanani maslahi ya binadamu na kutumia teknolojia za Akili Bandia kwa nia njema.

Kauli mbiu ya mkutano wa mwaka huu ni “Kujenga siku za baadaye za kidijitali za kutilia maanani maslahi ya binadamu na kutumia akili bandia kwa nia njema, kujenga pamoja jumuiya ya mtandao wa intaneti yenye mustakabali wa pamoja.” Mkutano huo umehusisha shughuli mbalimbali zikiwemo mabaraza madogo ya Pendekezo la Maendeleo ya Dunia, uchumi wa kidijitali na usimamizi wa teknolojia ya akili bandia.

Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mambo ya uchumi na ya kijamii Li Junhua alitoa hotuba kwa njia ya video kwenye ufunguzi wa mkutano huo kuwa, “Akili bandia inabadilisha maisha ya watu kwa kasi sana. Lazima tutilie maanani maslahi ya binadamu, kujua mahitaji na maoni ya watu wa duniani kote kwa kupitia mazungumzo, ili kutumia vizuri uwezo mkubwa wa akili bandia.”

Nii Narku Quaynor, Mkurugenzi mkuu wa Bodi ya wakurugenzi ya Kampuni ya Ghana Dot Com alisema, changamoto zinazoikabili Afrika ni kwa namna gani kuingiza tekolojia ya akili bandia, na kwa namna gani kuhakikisha Afrika inashiriki katika kuhuisha na kutumia teknolojia hiyo.

Kwenye mkutano wa baraza kuu uliofanyika mchana wa Jumatano Quaynor alisema, maeneo ya jamii na vitengo vya nafasi za mtandao wa intaneti za kikanda katika sehemu mbalimbali za Afrika zinafanya juhudi za uratibu ili kuleta miundombinu bora ya mawasiliano kwa bara hilo.

Mkutano wa Baraza kuu umesisitiza mambo muhimu mawili ya kuhimiza uvumbuzi wa teknolojia za akili bandia na kujenga siku za baadaye za kidijitali za kutilia maanani maslahi ya binadamu. Watu zaidi ya 1,800 wamehudhuria kwenye mkutano wa baraza kuu, wakiwemo wataalamu na waandishi wa habari kutoka mashirika ya kimataifa, idara za kiserikali na kampuni za intaneti za kuongoza.

Mkutano huo wa kilele umepangwa kufungwa leo Ijumaa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Deng Jie)

Picha