Lugha Nyingine
China na Brazil, Afrika Kusini na Umoja wa Afrika zimeanzisha kwa pamoja mpango wa ushirikiano wa kimataifa katika uwazi wa sayansi
China, Brazil, Afrika Kusini na Umoja wa Afrika kwa pamoja zimeanzisha kwa pamoja Mpango wa Ushirikiano wa Kimataifa katika uwazi wa Sayansi, kwa lengo la kujenga mazingira ya kimataifa yaliyo ya uwazi, haki, kutopendelea na yasiyobagua kwa maendeleo ya sayansi na teknolojia.
Hayo ni kwa mujibu wa Wizara ya Sayansi na Teknolojia ya China, ambapo imesema kuwa mpango huo pia unalenga kukuza uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia duniani ili kunufaisha Nchi za Kusini.
Mpango huo unapendekeza kwamba serikali, jumuiya za kisayansi, makampuni, mashirika yasiyo ya kiserikali na wadau wengine wanapaswa kuunga mkono mtiririko huru wa wafanyakazi wa uvumbuzi wa kisayansi na rasilimali kwa kiwango cha kimataifa, na kuhakikisha wadau mbalimbali wanaweza kushiriki kwa usawa na kutendewa kwa haki katika uwazi wa sayansi.
Mpango huo unasema kuwa serikali za nchi zote zinapaswa kuongeza uwekezaji katika uwazi wa sayansi na kuhimiza ushirikiano, ujenzi wa pamoja na kushirikiana kwa miundombinu mikuu ya utafiti wa kisayansi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma