Mapato ya huduma ya reli ya SGR ya Kenya yaongezeka kwa 36%

(CRI Online) Novemba 22, 2024

Picha hii iliyopigwa Septemba 20, 2023 ikionyesha treni inayoelekea Mombasa ikingoja kwenye Stesheni Kuu ya Nairobi ya reli ya SGR ya Mombasa-Nairobi iliyojengwa na China jijini Nairobi, Kenya. (Xinhua/Han Xu)

Shirika la Reli la Kenya (KRC) Alhamisi lilisema mapato ya huduma ya abiria ya reli ya SGR ya Kenya yameongezeka kwa asilimia 36 katika miezi tisa ya mwanzo ya mwaka 2024 licha ya idadi ya abiria kupungua.

Ripoti iliyotolewa na KRC imesema mapato hayo yamefikia dola milioni 22.3 za kimarekani ndani ya miezi tisa, likiwa ni ongezeko la dola milioni 16.4 za kimarekani ikilinganishwa na mwaka jana, huku idadi ya abiria waliosafiri kwa reli ya SGR ikifikia milioni 1.78, ambayo ni chini ikilinganishwa na idadi ya abiria milioni 1.95 ya mwaka jana wakati kama huo.

Ongezeko la mapato linatokana na kupandishwa kwa nauli na KRC kuanzia tarehe mosi Januari, ambayo imeongezeka kwa asilimia 50 kutokana na bei kubwa ya mafuta.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Deng Jie)

Picha