Lugha Nyingine
Rais wa Tanzania atembelea eneo la Jengo lililoporomoka wakati idadi ya vifo ikipanda hadi 20
(CRI Online) Novemba 22, 2024
Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania ametembelea eneo la jengo la ghorofa nne lililoporomoka la Kariakoo jijini Dar es Salaam, ambapo alitangaza kuwa idadi ya vifo imefikia 20.
Alipowasili kutoka Brazil, ambako alihudhuria mkutano wa kilele wa G20, rais Samia pia aliwatembelea watu walionusurika kwenye janga hilo katika hospitali ya taifa ya Muhimbili na kuwaombea kupona haraka. Amewaambia kuwa serikali itawasaidia mpaka wapone na kulinda mali zao zilizokuwa katika jengo hilo lililoporomoka.
Zaidi ya watu 86 waliokolewa wakati shughuli za uokoaji zikiingia siku ya tano Jumatano.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Deng Jie)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma