

Lugha Nyingine
Polisi nchini Kenya waua gaidi na kukamata silaha katika eneo la mpakani
Vikosi vya usalama vya Kenya vimeua gaidi mmoja na kukamata silaha kwenye operesheni iliyofanywa katika Kaunti ya Garissa, karibu na mpaka wa Somalia siku ya Jumamosi.
Kitengo cha Polisi wa Kupambana na Ugaidi kimesema wataalam wake wa Kundi la Operesheni Maalum (SOG) walifanya operesheni iliyoongozwa na intelijensia katika eneo la Najo la Fafi, wakikamata bunduki tatu aina ya AK-47 na magazini, chombo cha kurusha makombora cha RPG na kombora la RPG.
“Hatua hii inaashiria ushindi mwingine wa SOG katika kulinda taifa. Dhamira yao ya kuhakikisha usalama wa Wakenya wote inabaki kuwa thabiti” taarifa hiyo iliyotolewa na Kitengo cha Polisi wa Kupambana na Ugaidi imesema.
Kitengo hicho kimethibitisha kuwa operesheni hiyo imesababisha makabiliano kati yake na magaidi wa al-Shabab, na kimetoa wito kwa wananchi kuwa macho na mashambulizi ya wapiganaji wa kundi hilo linalotokea nchini Somalia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma