

Lugha Nyingine
Botswana mwenyeji wa mkutano wa kuendeleza maendeleo ya Afrika
Mkutano wa Uchumi wa Afrika ulioandaliwa kwa pamoja na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Kamisheni ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa kwa Afrika (ECA) na Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) umefanyika katika mji mkuu wa Botswana, Gaborone, mwishoni mwa wiki, Jumamosi.
Akizungumza kwenye mkutano huo, Rais wa Botswana Duma Boko amesema, ni muhimu kutumia kikamilifu Eneo la Biashara Huria la Afrika (AfCFTA) kuboresha biashara ya ndani ya Afrika na kuliweka bara hilo kuwa nguvu ya uchumi wa dunia.
Akielezea umuhimu wa Eneo hilo katika kubadili mazingira na mwenendo wa kiuchumi ya Afrika kwa kuchochea uwekezaji, kutoa nafasi za ajira na kuhimiza mageuzi ya kiviwanda, Rais Boko amesema ushirikiano wa kikanda ni lazima uende zaidi biashara kujumuisha uchangiaji wa miundombinu halisi, usimamizi wa rasilimali na utatuzi wa migogoro.
Katibu Mkuu wa ECA Claver Gatete amesema, AfCFTA ni ‘taji la dhahabu’ kwa juhudi za mafungamano ya kiuchumi za Afrika, akitoa wito wa kuongeza kasi ya utekelezaji wa eneo hilo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma