

Lugha Nyingine
China yatoa wito kwa nchi zilizoendelea kutimiza ahadi yao ya ufadhili kusaidia nchi zinazoendelea kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Mao Ning amesema, China inatoa wito kwa nchi zilizoendelea kutimiza kwa dhati wajibu wao katika kutoa uungaji mkono wa kifedha kwa nchi zinazoendelea ili kusaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi duniani.
Msemaji Mao ametoa wito huo jana Jumatatu wakati akijibu swali kuhusu Mkutano wa 29 wa Nchi Watia saini kwenye Makubaliano ya Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP29) ambao umemalizika Jumapili iliyopita Baku, Azerbaijan, kwa pande zote kufikia makubaliano kuhusu malengo mapya ya jumla ya kiasi cha fedha za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na maelezo ya utekelezaji wa Kifungu cha 6 cha Mkataba wa Paris.
Amesema China itaendelea kuimarisha ushirikiano wa Kusini na Kusini na kutoa uungaji mkono kwa nchi nyingine zinazoendelea katika kukabiliana na suala hilo kadri iwezavyo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma