Ziara ya Mkurugenzi Mtendaji wa Apple mjini Beijing yaonesha umuhimu wa mnyororo wa usambazaji na soko la China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 26, 2024

Mkurugenzi Mtendaji wa Apple Tim Cook akihudhuria hafla ya ufunguzi wa duka jipya kinara la Apple mjini Shanghai, Mashariki mwa China, Machi 21, 2024. (Xinhua/Liu Ying)

Mkurugenzi Mtendaji wa Apple Tim Cook akihudhuria hafla ya ufunguzi wa duka jipya kinara la Apple mjini Shanghai, Mashariki mwa China, Machi 21, 2024. (Xinhua/Liu Ying)

BEIJING - Katika ziara yake ya tatu katika China Bara mwaka huu, Mkurugenzi Mtendaji wa Apple Tim Cook alisema anathamini sana kampuni za usambazaji wa bidhaa wa China na wachambuzi wanaamini hii imeonyesha umuhimu wa mnyororo wa usambazaji na soko la China kwa kampuni hiyo ya Marekani.

"Ninajivunia kwamba Apple ina banda hapa na washirika wetu. Hatungeweza kufanya kile tunachofanya bila wao," Cook amesema Jumatatu kabla ya Maonyesho ya pili ya Kimataifa ya Mnyororo wa Usambazaji ya China (CISCE), yaliyopangwa kufanyika kuanzia leo Jumanne hadi Jumamosi mjini Beijing.

Kwenye ukumbi mkuu wa maonyesho hayo, Cook alitembelea banda la pamoja cha kampuni nne za usambazaji wa bidhaa za Apple za China, litakaloonyesha vipengele na teknolojia zinazohusika na mistari ya uzalishaji wa bidhaa za kunyumbulika, teknolojia ya kijani na bidhaa za lenzi. Amesisitiza uvumbuzi katika mnyororo wa usambazaji wa bidhaa wa Apple.

Wakati wa ziara yake mjini Shanghai mwezi wa Machi mwaka huu, Cook alisisitiza dhamira ya muda mrefu ya kampuni hiyo kwa soko la China alipofungua duka kubwa la Apple katika China Bara.

"Hakuna mnyororo wa usambazaji duniani ambao ni muhimu zaidi kwetu kuliko China," Cook amesema, akiongeza kuwa Apple itaimarisha ushirikiano wake wa muda mrefu na washirika wake wa usambazaji wa bidhaa wa China na kushirikiana nao kwa ukaribu katika nyanja za uzalishaji wa teknolojia za kijani na za kisasa ili kunufaishana.

Wakati akiwa ziarani mjini Beijing mwezi uliopita, Cook aliahidi kuendelea kuwekeza nchini China katika maeneo kama vile minyororo ya usambazaji na utafiti na uundaji wa bidhaa.

Wataalamu wanasema China ina fursa isiyolinganishwa katika utengenezaji, huku uwezo wake wa utafiti na uundaji bidhaa unaokua ukisaidia mvuto wa minyororo ya viwanda na usambazaji ya China.

Licha ya changamoto zikiwemo za hali ya nje isiyokuwa na uhakika, China bado ni sehemu isiyoepukika ya minyororo ya usambazaji duniani ya Apple. Kati ya kampuni 200 za usambazaji wa bidhaa za Apple duniani kote, asilimia zaidi ya 80 zimejenga viwanda nchini China, wakitengeneza bidhaa nyingi za Apple.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha