China yaahidi kuhakikisha utulivu wa minyororo ya viwanda na usambazaji duniani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 26, 2024

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akifanya kongamano na wawakilishi wa kampuni na mashirika yanayoshiriki katika Maonyesho ya pili ya Kimataifa ya Mnyororo wa Usambazaji ya China (CISCE), mjini Beijing, mji mkuu wa China, Novemba 25, 2024. (Xinhua/Wang Ye)

BEIJING - China itaendelea kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha minyororo ya viwanda na usambazaji duniani iliyo tulivu na isiyotatizika, Waziri Mkuu wa China Li Qiang amesema Jumatatu wakati akifanya kongamano na wawakilishi wa kampuni na mashirika yanayoshiriki katika Maonyesho yajayo ya pili ya Kimataifa ya Mnyororo wa Usambazaji ya China.

Waliohudhuria katika kongamano hilo ni wawakilishi wa kampuni za Apple Inc., Rio Tinto, Contemporary Amperex Technology na Baraza la Biashara la Marekani na China, miongoni mwa wengine.

Wakisisitiza imani yao katika uchumi wa China na matumaini yao juu ya fursa za soko la China, wawakilishi hao wamesema kampuni za kigeni nchini China zina nia ya kupanua uwekezaji wao na kuongeza maendeleo yao nchini humo, kuimarisha ushirikiano katika minyororo ya viwanda na ugavi duniani, na kupata matokeo ya kunufaisha pande zote.

Kwa upande wake Waziri Mkuu Li amesema kutokana na maendeleo ya kina ya utandawazi wa uchumi, minyororo ya viwanda na usambazaji duniani imepanuka hatua kwa hatua katika miongo michache iliyopita, ikihamasisha kukua kwa kasi uchumi wa dunia na kunufaisha pande zote.

“Wakati ukuaji wa uchumi wa dunia sasa unakosa nguvu, baadhi ya vitendo vya kujihami na hatua zinazozidisha dhana ya usalama zinaendelea kuharibu minyororo ya viwanda na usambazaji duniani, ikisukuma juu zaidi gharama za kampuni, kupunguza ufanisi wa uchumi na kuzuia kuendeleza kwa pamoja,” amesema.

Ametoa wito wa kufanya juhudi madhubuti za kulinda minyororo ya viwanda na usambazaji duniani iliyo imara na isiyotatizwa, vilevile maslahi ya pamoja ya pande mbalimbali.

Waziri Mkuu Li amesema kuwa China imepata ukuaji wa uchumi wa madhubuti kwa ujumla na kupiga hatua zaidi mwaka huu, akiongeza kuwa juhudi zaidi zitafanywa ili kuongeza kasi ya hatua za kukabiliana na mdororo na kuhimiza maendeleo mazuri ya uchumi.

Amesema China itaharakisha ujenzi wa mfumo wa kisasa wa viwanda, na kutoa uungaji mkono thabiti kwa ajili ya minyororo ya viwanda na usambazaji duniani kuendeshwa kwa ufanisi.

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akifanya kongamano na wawakilishi wa kampuni na mashirika yanayoshiriki katika Maonyesho ya pili ya Kimataifa ya Mnyororo wa Usambazaji ya China (CISCE), mjini Beijing, mji mkuu wa China, Novemba 25, 2024. (Xinhua/Wang Ye)

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akifanya kongamano na wawakilishi wa kampuni na mashirika yanayoshiriki katika Maonyesho ya pili ya Kimataifa ya Mnyororo wa Usambazaji ya China (CISCE), mjini Beijing, mji mkuu wa China, Novemba 25, 2024. (Xinhua/Wang Ye)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha