

Lugha Nyingine
Kenya yapanga kuanzisha soko la kaboni
Kenya inapanga kuanzisha soko la kaboni, ikiruhusu mashirika ya umma na ya binafsi kufanya biashara ya unit za upunguzaji utoaji hewa chafu, fidia na matokeo ya kupunguza athari za gesi chafu.
Katika taarifa yake iliyotolewa jijini Nairobi, mkurugenzi mtendaji na ofisa mtendaji mkuu wa Kampuni ya Uzalishaji Umeme nchini Kenya (KenGen) Peter Njenga amesema, jitihada hiyo inatarajiwa kuchochea ukuaji wa uchumi wa kaboni wa Kenya, ikifungua njia kwa nchi hiyo kubadili hatua za tabianchi kuwa za kuzalisha mapato kupitia uuzaji wa unit za kaboni.
Kwa mujibu wa KenGen, ambayo ni mjumbe wa kamati ya kiufundi ya sekta mbalimbali (MST) iliyopewa jukumu la kuunda mfumo wa soko la kaboni la nchi hiyo, Kenya tayari imeunda muundo wa kiufundi kusimamia maendeleo ya miradi ya kaboni na kuhamasisha ushiriki katika masoko ya kaboni.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma