UN yahitimisha warsha ya kuimarisha udilifu wa uchaguzi nchini Sudan Kusini

(CRI Online) Novemba 26, 2024

Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS) imesema imekamilisha warsha ya siku mbili kwa waendesha mashtaka na wapelelezi wa Polisi 50 ili kukabiliana na makosa ya kiuchaguzi na kudhibiti hali za uwezekano wa vurugu za kiuchaguzi kuathiri uadilifu wa mchakato wa uchaguzi.

Katika taarifa yake, UNMISS imesema, warsha hiyo iliyokutanisha washiriki kutoka majimbo ya Bahr El Ghazal Magharibi, Bahr El Ghazal Kaskazini, Warrap na Lakes, imelenga kujenga uwezo wa taasisi husika na kutoka mapendekezo ya namna zipaswa kuitikia uwezekano wa ukiukaji wa kanuni za uchaguzi.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na Masuala ya Kikatiba wa nchini humo Gabriel Isaac Awow amesema, kuhakikisha uadilifu wa uchaguzi nchini Sudan Kusini ni msingi mkuu wa demokrasia.

“Warsha hii inawapa waendesha mashtaka na wapelelezi wa Polisi uzoefu hitajika kubaini, kuzuia na kuitikia makosa ya kiuchaguzi, ambayo ni muhimu katika kudumisha imani ya umma katika mchakato wa uchaguzi” amesema.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha