Lugha Nyingine
Fika Shenzhen, China uone papa nyangumi mecha anayecheza na samaki
Katika Eneo la Burudani za Dunia ya Bahari la Xiaomeisha Shenzhen , mkoani Guangdong, China watembeleaji wanaweza kuona papa nyangumi mecha wa kutengenezwa na binadamu. Ana urefu wa mita 4.7, na umbo lake kuu limetengenezwa kwa aloi ya titani ya TC4 na chuma cha 316L kisicho na madoa. Aliundwa kwa sehemu na vipuri 13,000 vilivyotengenezwa kwa usahihi zaidi, na ana vifaa vihisi 156 ndani yake, ambavyo vinaweza kuigilizia mijongeo dhahiri ya papa nyangumi halisi wanaoogelea ndani ya maji.
Papa nyangumi huyo si tu anaonyesha teknolojia ya hali ya juu ya viumbe vya kutengenezwa na binadamu kwa kuigilizia viumbe halisi, lakini pia kupunguza hali yake ya kutegemea kuonesha viumbe halisi wa baharini, ikisaidia watembeleaji kuelewa umuhimu wa ikolojia ya baharini na kulinda viumbe vilivyo hatarini kutoweka.
Taihe, Jiangxi, China: Ujenzi wa Daraja la Chengjiang waendelea kwa kasi
Mawimbi ya Baridi Kali Yaikumba China, Maeneo Mengi Yashuhudia Kuanguka kwa Theluji
Theluji yaanguka kwa mara ya kwanza mwaka huu kwenye Milima Emei, China
Mkutano wa 19 wa Viongozi wa Kundi la 20 (G20) kufanyika Rio de Janeiro
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma