Bunge la Ulaya laidhinisha Kamati Mpya ya Ulaya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 28, 2024
Bunge la Ulaya laidhinisha Kamati Mpya ya Ulaya
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulaya Ursula von der Leyen akihudhuria mkutano na waandishi wa habari baada ya upigaji kura katika makao makuu ya Bunge la Ulaya huko Strasbourg, Ufaransa, Novemba 27, 2024. (Xinhua/Zhao Dingzhe)

STRASBOURG, Ufaransa - Bunge la Ulaya limeidhinisha timu mpya ya Kamati ya Ulaya jana Jumatano, inayoongozwa na Ursula von der Leyen wa Ujerumani, ambaye atahudumu kwa awamu yake ya pili ya miaka mitano akiwa mwenyekiti wa kamati hiyo, ambapo wabunge wameidhinisha kamati hiyo kwa kura 370 za ndiyo, 282 za hapana, na 36 za kuachwa , ikitoa taa ya kijani kwa timu hiyo ya watendaji 27.

Janis Emmanouilidis, naibu mtendaji mkuu wa Kituo cha Sera cha Ulaya, amesema kamati hiyo mpya inaonyesha “nguvu ya mwenyekiti” iliyoimarishwa, ambapo wajumbe wa kamati hiyo wanashirikiana na von der Leyen kwenye kiwango cha juu. Tofauti na hali ya awamu iliyopita, sauti ya upinzani kama zimetoweka. Emmanouilidis amesisitiza umuhimu wa kudumisha "baraza la mawazirilenye nguvu", ingawa kamati mpya inaendelea kuongozwa na mwenyekiti huyo huyo mwenye nguvu wakati wa kukabiliwa na changamoto nyingi.

Mbunge wa zamani wa Poland Jacek Saryusz-Wolski amekosoa uidhinishaji huo wa kamati mpya kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, akiuita "uidhinishaji wa kura chache kabisa wa Bunge la Ulaya katika historia" na akidai matokeo hayo yamechochewa na "mapatano kati ya vyama."

Von der Leyen alitoa hotuba kabla ya upigaji huo wa kura siku ya Jumatano. Katika hotuba yake hiyo, von der Leyen alizindua Dira ya Ushindani, ikiashiria mpango mkuu wa kwanza wa Baraza jipya la Makamishna.

Mpango huo umewekwa kwenye msingi wa nguzo tatu muhimu: kuziba pengo la uvumbuzi, kutekeleza mpango wa pamoja wa kuondoa kaboni na kuwa na nguvu ya ushindani ya pamoja , na kuimarisha usalama huku ukipunguza utegemezi, von der Leyen amesema.

"Sisi ni takriban sawa na Marekani katika kuanzisha kampuni mpya za kiteknolojia. Lakini linapokuja suala la upanuzi wa kampuni hizo, tunafanya vibaya zaidi kuliko washindani wetu," von der Leyen amesema, akisisitiza ahadi ya kamati hiyo mpya ya kuongeza uwekezaji na mkazo wake zaidi wa kimkakati kwenye uvumbuzi.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha