Ethiopia yaandaa maonyesho ya kwanza ya vyombo vya usafiri vinavyotumia umeme ili kuendeleza matumizi ya vyombo vya nishati ya kijani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 28, 2024
Ethiopia yaandaa maonyesho ya kwanza ya vyombo vya usafiri vinavyotumia umeme ili kuendeleza matumizi ya vyombo vya nishati ya kijani
Wafanyabiashara wakionyesha magari yanayotumia umeme kwenye maonyesho ya Ethio-Green Mobility 2024 mjini Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, Novemba 25, 2024. (Xinhua/Michael Tewelde)

ADDIS ABABA - Ethiopia imeandaa maonyesho yake ya kwanza kabisa ya vyombo vya usafiri na uchukuzi vinavyotumia nishati ya kijani yajulikanayo kwa jina la Ethio-Green Mobility 2024 ikiwa ni sehemu ya dhamira yake ya kupunguza utoaji wa hewa ya kaboni na kuhimiza suluhu za usafiri wa kijani.

Yakiwa yalianza Novemba 22 na yamepangwa kuendelea hadi Jumamosi katika Eneo Maalum la Kimataifa la Kiuchumi la Viwanda Vyepesi la Huajian huko Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, maonyesho hayo yanaonyesha ubunifu na teknolojia mpya katika vyombo vya usafiri vinavyotumia nishati ya kijani, ikiwa ni pamoja na magari ya kisasa yanayotumia umeme (EVs) na teknolojia za nishati mbadala.

Akihutubia maonyesho hayo, Waziri wa Uchukuzi na Lojistiki wa Ethiopia Alemu Sime ameyazungumzia maonyesho hayo kuwa ni sehemu ya dhamira ya serikali ya kuendeleza matumizi ya vyombo vya usafiri endelevu na kujenga uchumi wa kijani unaohimili tabianchi.

Sime amesema kuwa Ethiopia inafanya kazi kwa bidii ili kupunguza utegemezi wake kwa nishati zisizo mbadala katika sekta ya usafiri kwa kutumia rasilimali zake nyingi za nishati mbadala.

Maonyesho hayo, yanayovutia wafanyabiashara wengi kutoka China, hutumika kama jukwaa la kuunda mitandao na kuwezesha muunganisho wa soko kati ya kampuni na wateja wanaohusika katika vyombo vya usafiri vyenye kutumia nishati ya kijani.

Li Xuan, mwakilishi wa kampuni ya magari ya EV ya China, Neta nchini Ethiopia, ameshuhudia ongezeko la mahitaji ya EVs nchini Ethiopia baada ya mpango wa serikali wa kupunguza uagizaji wa magari yanayotumia gesi.

"Bidhaa nyingi za EV zinazotengenezwa nchini China zinauzwa nchini Ethiopia ambapo soko la EVs linastawi baada ya mpango wa serikali wa kupiga marufuku uagizaji wa magari yanayotumia petroli," Li amelimbia Shirika la Habari la China, Xinhua.

Ukiacha magari ya umeme, baiskeli zinazotumia umeme na bajaji za magurudumu matatu pia zimevutia watembeleaji wengi kwenye maonyesho hayo.

Magari zaidi ya 100,000 za umeme sasa yanatumika kote Ethiopia, wakati mamlaka zinataka kuongezeka hadi 500,000 katika miaka 10 ijayo, zikiwa mbadala wa asilimia 95 ya magari yanayotumia nishati ya mafuta.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha