Rais Xi Jinping asisitiza maendeleo yenye ubora wa juu ya ushiriki wa utoaji na uuzaji wa bidhaa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 29, 2024

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amehimiza ushiriki wa utoaji na uuzaji bidhaa kuonesha umuhimu wake kama madaraja, ili Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na serikali kudumisha mawasiliano ya karibu na wakulima, na kujitahidi kuandika ukurasa mpya wa maendeleo yenye ubora wa juu ya ushiriki wa utoaji na uuzaji wa bidhaa.

Rais Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), amesema hayo katika maagizo yake kwenye maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Shirikisho Kuu la Ushiriki wa Utoaji na Uuzaji wa Bidhaa la China.

Shirikisho kuu hilo lililoanzishwa mwaka 1954, ni shirika la kiuchumi la kitaifa linalohusika na kuandaa, kuratibu na kusimamia uendeshaji wa raslimali muhimu za uzalishaji wa kilimo, pamoja na mazao ya kilimo na bidhaa zake.

“Katika miongo saba iliyopita, ushiriki wa utoaji na uuzaji bidhaa nchini China umefanya kazi kubwa katika kuhudumia wakazi wa vijijini na mijini, kuhimiza ukuaji wa uchumi wa vijijini, kusaidia kutokomeza hali ya umaskini zaidi, kuinua mapato ya wakulima na kuhimiza ustawishaji wa vijiji ,” Rais Xi amesema.

Amezitaka kamati za Chama na serikali za ngazi zote kuimarisha zaidi kuongoza na kuunga mkono kazi ya ushiriki wa utoaji na uuzaji bidhaa.

Rais Xi amehimiza ushiriki wa utoaji na uuzaji bidhaa kujenga majukwaa jumuishi ambayo yanahudumia uzalishaji na maisha ya wakulima na kusaidia kuhimiza maendeleo ya kilimo cha kisasa.

Waziri Mkuu wa China Li Qiang, ambaye pia ni mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC, pia ametoa maagizo kuhusu ushiriki wa utoaji na uuzaji bidhaa.

Waziri Mkuu Li amehimiza ushiriki wa utoaji na uuzaji bidhaa kusukuma mbele zaidi maendeleo yenye ubora wa juu ya mazao ya kilimo na bidhaa zake, mzunguko wa usambazaji wa mazao ya kilimo, pamoja na kuchakata na kutumia kikamilifu rasilimali mbadala.

Mkutano umefanyika Beijing jana siku ya Alhamisi kuadhimisha miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Shirikisho Kuu la Ushiriki wa Utoaji na Uuzaji wa Bidhaa.

Mkutano ukifanyika kuadhimisha miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Shirikisho Kuu la Ushiriki wa Utoaji na Uuzaji wa Bidhaa la China  katika mji mkuu wa China Beijing, Novemba 28, 2024. (Xinhua/Ding Haitao)

Mkutano ukifanyika kuadhimisha miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Shirikisho Kuu la Ushiriki wa Utoaji na Uuzaji wa Bidhaa la China katika mji mkuu wa China Beijing, Novemba 28, 2024. (Xinhua/Ding Haitao)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha