Lugha Nyingine
Vituo vya utafiti na maendeleo vya nchi za nje mjini Beijing vyarekodi kuongezeka kwa matumizi ya utafiti na maendeleo katika mwezi Januari hadi Agosti
Picha hii iliyopigwa kutoka Kilima Jingshan Agosti 12, 2024 ikionyesha maghorofa marefu ya eneo la kati la kibiashara (CBD) mjini Beijing, mji mkuu wa China. (Xinhua/Li Xin)
BEIJING – Vituo vikubwa jumla ya 121 vya utafiti na maendeleo (R&D) vinavyowekezwa kwa mtaji wa kigeni mjini Beijing, China vimewekeza yuan bilioni 13.77 (dola za kimarekani bilioni 1.92) kwenye kazi za utafiti na maendeleo katika miezi minane ya kwanza ya Mwaka 2024, ikiwa ni ongezeko la asilimia 29.9 mwaka hadi mwaka, mamlaka za Mji wa Beijing zimesema jana Alhamisi.
Mji wa Beijing kwa sasa una makao makuu ya kikanda 252 ya kampuni za kimataifa na vituo 149 vya utafiti na maendeleo vinavyowekezwa kwa mtaji wa kigeni, serikali ya mji wa Beijing imesema.
Li Yang, katibu mkuu wa Shirikisho la Kampuni zinazowekezwa na nchi za nje la Beijing, amesema kuwa kampuni kubwa za kigeni zina matumaini kuhusu ukuaji wa muda mrefu wa uchumi wa China na zinaendelea kuichukulia nchi hiyo kama sehemu pendelewa zaidi ya uwekezaji.
Ili kuboresha zaidi mazingira yake ya biashara, serikali ya Beijing imetekeleza hatua zaidi ya 1,500 za mageuzi na kutengeneza upya kanuni zake za kuboresha mazingira ya biashara katika miaka michache iliyopita.
Julai 1 mwaka huu, kanuni maalum ya kwanza ya Beijing juu ya uwekezaji wa nchi za nje ilianza kutekelezwa, ikionyesha juhudi za mji huo kuhimiza ufunguaji mlango zaidi na kuongeza mvuto wake kwa wawekezaji wa kimataifa.
Taihe, Jiangxi, China: Ujenzi wa Daraja la Chengjiang waendelea kwa kasi
Mawimbi ya Baridi Kali Yaikumba China, Maeneo Mengi Yashuhudia Kuanguka kwa Theluji
Theluji yaanguka kwa mara ya kwanza mwaka huu kwenye Milima Emei, China
Mkutano wa 19 wa Viongozi wa Kundi la 20 (G20) kufanyika Rio de Janeiro
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma