China yataka Marekani kuondoa mfumo wa makombora kutoka Ufilipino

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 29, 2024

BEIJING - Wu Qian, Msemaji wa Wizara ya Ulinzi wa Taifa ya China siku ya Alhamisi ametaka kuondolewa mara moja kwa mfumo wa makombora ya Typhon ya masafa ya kati wa Marekani kutoka Ufilipino.

Wu, amesema hayo wakati akijibu swali la vyombo vya habari kuhusu habari za hivi punde kwamba Ufilipino inafikiria kununua mfumo huo wa makombora kutoka Marekani.

“China imesema mara kwa mara kwamba inapinga Marekani kuweka mfumo huo wa makombora ya masafa ya kati nchini Ufilipino,” Wu amesema.

Akiutaja mfumo huo wa makombora wa Kimbunga "silaha ya mashambulizi," Wu amesema Ufilipino kukubali Marekani kuweka mfumo huo kumeongeza mapambano ya kisiasa ya kijiografia na kuzidisha mvutano katika kanda.

Hili kwa vyovyote si jambo la Ufilipino pekee; linahusu usalama wa pamoja wa nchi zote katika kanda, Wu amesema.

"Historia na hali halisi ya hivi sasa zimethibitisha mara kwa mara kwamba mahali ambapo kuna silaha za Marekani zimewekwa, kutakuwa na hatari kubwa ya migogoro," amesema.

"Tunazitaka pande husika kuondoa mara moja mfumo wa makombora ya Typhon ya masafa ya kati ," msemaji amesema, akisisitiza kwamba ikiwa Marekani na Ufilipino zitasisitiza kuendelea kufuata njia hiyo ya makosa, upande wa China utachukua hatua za kithabiti kwa kuizuia.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha