Afrika Kusini ina dhamira ya kutokomeza umaskini kupitia hatua za pamoja: Rais Ramaphosa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 29, 2024

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini akitoa hotuba yake ya mwaka kwa Baraza la Taifa la Majimbo la Afrika Kusini (NCOP) mjini Cape Town, Afrika Kusini, Novemba 28, 2024. (Picha na Xabiso Mkhabela/Xinhua)

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini akitoa hotuba yake ya mwaka kwa Baraza la Taifa la Majimbo la Afrika Kusini (NCOP) mjini Cape Town, Afrika Kusini, Novemba 28, 2024. (Picha na Xabiso Mkhabela/Xinhua)

CAPE TOWN - Afrika Kusini ina dhamira ya kutokomeza umaskini nchini humo kupitia hatua za pamoja na mageuzi makubwa ya kijamii na kiuchumi, Rais Cyril Ramaphosa amesema mjini Cape Town, mji mkuu wa kibunge wa Afrika Kusini alipokuwa akitoa hotuba yake ya mwaka kwa Baraza la Taifa la Majimbo (NCOP), ambalo ni baraza la juu la bunge la nchi hiyo.

Hotuba na mjadala kuhusu suala hilo umefanyika chini ya kaulimbiu ya "Kudhamiria Jitihada Zetu katika Kupunguza Umaskini na Kukabiliana na Gharama Kubwa za Maisha."

"Kama utumwa na ubaguzi wa rangi, umaskini si wa kiasili. Umesababishwa na binadamu na unaweza kukabiliwa na kukomeshwa na hatua za binadamu," Ramaphosa ametangaza, akirejelea maneno ya Nelson Mandela.

Amesema kuwa umaskini nchini Afrika Kusini una mizizi iliyokita kwa kina, ikiwa ni pamoja na karne nyingi za udhalilishaji, kunyang'anywa mali na kutengwa na ukoloni na ubaguzi wa rangi.

"Kwa hivyo kutokomeza umaskini na ukosefu wa usawa nchini Afrika Kusini ni lazima kufanya mageuzi ya kimsingi ya kijamii na kiuchumi ya nchi yetu," amesema.

Ramaphosa pia ameelezea maendeleo ya serikali katika kuondoa mamilioni ya Waafrika Kusini kutoka kwenye umaskini uliokithiri. Kwa mujibu wake, mwaka 1993, asilimia 71 ya Waafrika Kusini walikuwa wakiishi katika umaskini, hadi mwaka 2010 kiwango hicho cha umaskini kilikuwa kimeshuka hadi asilimia 61 na mwaka 2020, kilikuwa kimefikia asilimia 56.

Ramaphosa amekiri kuwa changamoto bado zipo, kutokana na kwamba karibu robo ya watu nchini humo wanakumbwa na umaskini wa chakula, na ukosefu wa ajira, hasa miongoni mwa vijana, ukiendelea kuwa changamoto kubwa.

Ili kukabiliana na changamoto hizo, "lengo letu ni juu ya hatua tunazopaswa kuchukua -- kwa ujasiri na kwa uharaka -- kutekeleza mamlaka yetu ya kuchaguliwa," amesema. "Hatua zetu lazima zilete mabadiliko halisi katika maisha ya watu sasa. Hatua zetu lazima pia zijenge uchumi jumuishi ambao utaendelea kupunguza umaskini katika siku zijazo -- na hatimaye kuutokomeza."

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini akiwasili bungeni kutoa hotuba yake ya mwaka kwa Baraza la Taifa la Majimbo (NCOP) mjini Cape Town, Afrika Kusini, Novemba 28, 2024. (Picha na Xabiso Mkhabela/Xinhua)

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini akiwasili bungeni kutoa hotuba yake ya mwaka kwa Baraza la Taifa la Majimbo (NCOP) mjini Cape Town, Afrika Kusini, Novemba 28, 2024. (Picha na Xabiso Mkhabela/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha