China Bara yakosoa vikali Marekani kuiuzia Taiwan silaha na kuonya matokeo mabaya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 02, 2024

BEIJING - Msemaji wa China Bara amekosoa vikali Marekani kuiuzia Taiwan silaha na kulaani vikali jaribio lake la kulifanya kisilaha eneo hilo.

Chen Binhua, msemaji wa Ofisi ya Masuala ya Taiwan ya Baraza la Serikali la China, ameyasema hayo jana Jumapili wakati akijibu Marekani kutangaza kuidhinisha kuiuzia Taiwan silaha yenye thamani ya dola milioni 385.

Chen pia amekosoa watawala wa Chama cha Kidemokrasia cha Maendeleo cha Taiwan, akisema kuwa kulipa "ada za ulinzi" hakutaipa Taiwan usalama wowote, bali kujiangamiza yenyewe.

"Acheni kuomba uungwaji mkono wa Marekani kwa 'Taiwan kujitenga' kwani juhudi kama hizo zinaelekea kushindwa," ameongeza.

Chen amesema hatua hiyo ya Marekani hailingani kabisa na ahadi ya viongozi wa Marekani ya kutounga mkono "Taiwan kujitenga" na inakiuka vibaya kanuni ya kuwepo kwa China moja na taarifa tatu za pamoja za China na Marekani, hasa Taarifa ya Agosti 17, Mwaka 1982.

Msemaji huyo ameitaka Marekani kuacha mara moja kuiuzia Taiwan silaha. "Usidharau kamwe azma ya China ya kuchukua hatua kali za kulipiza ili kulinda kithabiti mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi " ameongeza. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha