

Lugha Nyingine
Sera ya China ya kusamehe visa kwa wageni wanaoingia yaonyesha ufunguaji mlango zaidi
Watalii kutoka Uswizi wakiwa kwenye picha ya pamoja mbele ya Jumba la Maombi ya Mavuno Mema, au Qiniandian, katika Bustani ya Tiantan (Hekalu la Mbinguni) mjini Beijing, mji mkuu wa China, Julai 9, 2024. (Xinhua/Ju Huanzong)
BEIJING - Kupanua sera ya kusamehe visa kwa wageni wanaoingia ni hatua muhimu katika safari ya China kufungua mlango zaidi na pia inaonyesha imani yake katika jukwaa la kimataifa.
Kuanzia Jumamosi, China ilipanua sera yake hiyo ya upande mmoja ya kusamehe visa kwa wamiliki wa pasipoti za kawaida kutoka nchi tisa zaidi. Hadi sasa, sera hiyo ambayo iko katika majaribio imetumika kwa nchi 38 tangu kuzinduliwa kwake mwaka mmoja uliopita.
Wakati huo huo, China imetia saini makubaliano ya kusameheana visa ya pande mbili na nchi 157, yanayohusisha aina tofauti za pasipoti.
Msimamo rasmi wa serikali ya China ni kwamba, China haitafunga mlango wake lakini badala yake itaufungua zaidi kwa nchi za nje. Sera hiyo pia imetekelezwa kwa hatua halisi na zenye ufanisi.
Wachambuzi wanasema kwamba, sera hiyo ni hatua kubwa katika kuwezesha mawasiliano kati ya watu na ya kibiashara na kuendeleza ufunguaji mlango wa kiwango cha juu. Ufunguaji mlango zaidi utanufaishana.
Aidha, wanasema kuwa, usafiri rahisi wa kuvuka mpaka unaongeza kasi ya ukuaji na ustawi wa uchumi wa China. Wakati huo huo, soko kubwa la China linatoa fursa nyingi za ushirikiano wa kibiashara wa kunufaishana na kuukuaji na nchi zingine.
Wageni kutoka nchi mbalimbali wanaowasili nchini China wameongezeka kutokana na hatua hizo. Katika robo ya tatu ya Mwaka 2024, watu karibu milioni 8.2 kutoka nchi za nje wamekuja China kutalii, ikiwa ni ongezeko la asilimia 48.8 mwaka hadi mwaka. Kati ya hizo takriban watu milioni 4.9 waliingia bila kuhitaji visa, ikiwa ni ongezeko la asilimia 78.6 kuliko mwaka jana kipindi kama hicho.
Sera hiyo ya China ya kusamehe visa inalingana sana na methali ya Confucian yenye historia ya miaka 2,500: "Ni furaha sana kuwa na marafiki wanaokuja kutoka mbali."
Kupanua nchi zinazonufaika na sera hiyo ya kusamehe visa na hatua nyingine zinaendana na wito wa China wa kujenga uchumi wa dunia wenye sifa za ushirikiano, uwazi na uvumbuzi, miongoni mwa mambo mengine.
Sera za hivi karibuni za China, kama vile kuondoa vizuizi vyote kwa wawekezaji wa kigeni katika viwanda na kuruhusu kuanzishwa kwa hospitali zinazomilikiwa na wageni kikamilifu katika miji iliyochaguliwa, zinaonesha azma ya China katika kufuata utandawazi wa uchumi ambao una hamasa zaidi, jumuishi na endelevu kupitia juhudi za pamoja na nchi nyingine.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma