Waziri Mkuu wa Iraq na Rais wa Iran wajadili hali ya Syria na Palestina

(CRI Online) Desemba 02, 2024

Waziri Mkuu wa Iraq Bw. Mohammed Shia' al-Sudani na Rais Masoud Pezeshkian wa Iran wamefanya mazungumzo jana Jumapili kushughulikia mivutano inayoongezeka kwenye eneo la Mashariki ya Kati, ikiwemo migogoro ya Gaza na nchini Syria, kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya al-Sudani.

Katika mazungumzo hayo ya simu, viongozi hao wawili wamesisitiza haja ya kuimarisha ushirikiano wa kikanda ili kusimamisha vita huko Gaza, na kuzuia uvunjifu wa amani na utulivu zaidi nchini Syria, wakionya kuwa machafuko hayo yanayoendelea yanaweza kutishia usalama na utulivu wa kikanda.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha