

Lugha Nyingine
Kenya yatoa wito wa ufuataji makini wa hatua za kuzuia Mpox huku visa vikiongezeka
(CRI Online) Desemba 02, 2024
Wizara ya Afya ya Kenya imetoa wito kwa watu kuzingatia kwa makini hatua za kuzuia ugonjwa wa Mpox wakati ambapo idadi ya watu wanaoambukizwa ikiendelea kuongezeka, huku watoto wakiwa hatarini zaidi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ya Kenya Bibi Mary Muthoni, amesema katika taarifa iliyotolewa Nairobi Jumapili kwamba, wagonjwa watano wapya wamethibitishwa kaskazini-magharibi, pwani na katikati ya Kenya katika wiki iliyopita, ikifanya jumla ya idadi ya watu walioambukizwa kuwa 23.
Bibi Muthoni amesema watoto, hasa wale wenye umri wa chini ya miaka mitano wako hatarini zaidi, kwa hiyo wizara ya Afya inasisitiza umuhimu wa kuwa mbali na watu wanaoshukiwa au waliothibitishwa kuambukizwa, ili kuepusha maambukizi kwa watoto.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma