

Lugha Nyingine
Ushirikiano kati ya Zimbabwe na China katika rasilimali watu waimarisha kulea vipaji nchini Zimbabwe
Balozi wa China nchini Zimbabwe Zhou Ding akizungumza kwenye tafrija kwa ajili ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Rasilimali Watu kati ya China na Zimbabwe mjini Harare, Zimbabwe, Novemba 29, 2024. (Picha na Tafara Mugwara/Xinhua)
HARARE - Ushirikiano kati ya Zimbabwe na China katika maendeleo ya rasilimali watu umekuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha mafunzo ya ufundi stadi katika nchi hiyo, Waziri wa Nchi anayeshughulikia Masuala ya Majimbo na Ugatuzi wa Jimbo la Mashonaland Mashariki nchini Zimbabwe, Apollonia Munzverengwi amesema Ijuma kwenye tafrija ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Rasilimali watu kati ya China na Zimbabwe iliyofanyika katika Ubalozi wa China mjini Hararenchini Zimbabwe.
Munzverengwi amesema ushirikiano kati ya pande hizo mbili katika maendeleo ya rasilimali watu, unaimarisha uhusiano uliopo kati ya pande mbili.
Amekumbushia ushiriki wake katika warsha ya mawaziri kuhusu kilimo cha kidijitali na ustawishaji wa vijijini nchini China, ambapo ujumbe wa Zimbabwe unaojumuisha maofisa wa serikali ulipata mafunzo muhimu kutokana na maendeleo ya China katika maeneo ya vijijini kupitia ustawishaji wa vijijini.
Munzverengwi amesema wamejifunza mengi na wamejipanga kutekeleza baadhi ya maarifa waliyopata, hivyo kuziba pengo kati ya matajiri na maskini nchini Zimbabwe.
"Lilikuwa jambo la kufumbua macho. Tulijifunza mengi, tulitembelea miji ya kisasa, tulitembelea jumuiya za ushirika, tulitembelea kituo cha utafiti, na kurudi nyumbani na mawazo ambayo tunakusudia kutekeleza katika majimbo yetu," amesema.
Katika hotuba yake kwenye tafrija hiyo, Balozi wa China nchini Zimbabwe Zhou Ding amesema ushirikiano wa maendeleo ya rasilimali watu siku zote umekuwa sehemu muhimu ya uhusiano kati ya China na Zimbabwe.
Zhou amesema katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, Wazimbabwe takriban 700 kutoka sekta mbalimbali wameshiriki katika programu mbalimbali za mafunzo na mawasiliano nchini China, zikiwemo elimu, mambo ya fedha, kilimo, afya, utawala wa umma, kupunguza umaskini, diplomasia, utalii, reli, uchumi wa kidijitali, na maendeleo ya kijani.
Grasiano Nyaguse, Konsuli wa Ubalozi wa Jamhuri ya Zimbabwe nchini China, akitembelea banda la kilimo cha kisasa cha kupanda mimea bila udongo la Kampuni ya Kilimo cha Kisasa ya Guizhou Aerospace mjini Guiyang, Mkoani Guizhou, kusini-magharibi mwa China, Juni 4, 2024. (Xinhua/Wu Si)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma