

Lugha Nyingine
Algeria yaanzisha mradi wa dola za kimarekani bilioni 2.33 kuongeza uzalishaji wa gesi
Kampuni ya nishati ya Serikali ya Algeria Sonatrach imeanzisha mradi wenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 2.33 ili kuongeza uzalishaji wa gesi katika kisima cha Hassia Rmel kilichoko Jimbo la Laghouat.
Kampuni hiyo imesema, mradi huo unalenga kudhibiti upotevu wa gesi katika uchimbaji na usafirishaji na kudumisha kiwango cha uzalishaji wake wa kila siku katika mita za ujazo milioni 188, na unahusisha ujenzi wa vituo vitatu vya kubana gesi vikiwa na kampresa 20 na uboreshaji mfumo wa mtandao wa kukusanya gesi.
Kwa mujibu wa kampuni hiyo, kituo cha eneo la kati cha kuongeza nguvu ya usafirishaji wa gesi kinatarajiwa kuanza kufanya kazi Oktoba 2026, kikifuatiwa na vituo vya maeneo ya kaskazini na kusini, mtawalia, kati ya Januari na Aprili mwaka 2027.
Mkurugenzi wa Sonatrach,Tawi la Hassi Rmel, Bw. Youcef Loucif amesema mradi huo utasaidia kurejesha akiba ya ziada ya gesi kavu yenye ujazo wa mita za ujazo bilioni 121, tani milioni 7 za gesi ya kimiminika, na tani milioni 3 za gesi kimiminika ya petroli (LPG).
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma