

Lugha Nyingine
Elimu ya mtandaoni yakabiliwa na changamoto nchini Sudan kufuatia kukatika kwa umeme na intaneti
Elimu ya mtandaoni, ambayo ni rasilimali muhimu kwa wanafunzi katika maeneo yaliyoathiriwa na vita nchini Sudan, inakabiliwa na changamoto kutokana na kukatika mara kwa mara kwa huduma za umeme na intaneti.
Vita vimeharibu miundombinu ya elimu jimboni Khartoum, ambako shule nyingi zimebadilishwa kuwa kambi za jeshi, ikisababisha wanafunzi wa maeneo hayo kutoweza kurudi katika madarasa ya kawaida.
“Wanafunzi wengi wana utayari wa kutumia majukwaa ya kielektroniki, lakini kukosekana kwa utulivu wa huduma za umeme na muunganisho mbaya wa intaneti vinafanya ushiriki wenye ufanisi karibia usiwezekane” Mjumbe wa bodi ya shule za binafsi za Al-Fath, Bw. Ayman Hassan Mohamedain amesema
Kwa mujibu wa UNICEF, watoto karibu milioni 17 nchini Sudan wako nje ya mfumo wa elimu kutokana na vita vinavyoendelea.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma