China yaitaka Marekani kuacha kusaidia na kuchochea nguvu ya kuifanya "Taiwan Ijitenge"

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 03, 2024

BEIJING - Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Lin Jian amesema jana Jumatatu kuwa, China inaitaka Marekani kuacha kusaidia na kuchochea nguvu ya kuifanya "Taiwan ijitenge".

Lin alisema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari alipotakiwa kutoa maoni yake kuhusu kiongozi wa Taiwan Lai Ching-te aliyeongea kwa njia ya simu na Spika wa zamani wa Bunge la Marekani Nancy Pelosi wakati Lai akiwa katika ziara ya Pasifiki pamoja na kutua huko Hawaii.

Lin amesema China inapinga kithabiti aina yoyote ya mawasiliano rasmi kati ya Marekani na eneo la Taiwan, na inapinga kithabiti aina yoyote ya vitendo vya Marekani vya kusaidia au kuchochea watu wanaofanya shughuli za mafarakano kuifanya "Taiwan ijitenge".

Suala la Taiwan ni kiini cha maslahi ya msingi ya China, na pia ni mstari wa kwanza mwekundu ambao hauruhusiwi kuvukwa katika uhusiano wa China na Marekani, Lin amesema.

Ameihimiza Marekani kuiona vya kutosha hali halisi ya kufanya mafarakano ya Lai Ching-te na watawala wa Chama cha Kidemokrasia cha Maendeleo, kuelewa vya kutosha madhara mabaya ya shughuli za mafarakano ya makundi ya kutaka “Taiwan ijitenge" kwa amani na utulivu katika Mlango wa Bahari wa Taiwan, kufuata kwa pande zote kanuni ya kuwepo kwa China moja na taarifa tatu za pamoja za China na Marekani, na kuacha kuingilia mambo yanayohusiana na Taiwan, kwani hayo ni mambo ya ndani ya China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha