UNAIDS yatoa mwito wa kuboreshwa huduma za afya kwa watu wenye VVU waliopoteza makazi nchini Ethiopia

(CRI Online) Desemba 03, 2024

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na UKIMWI (UNAIDS) limetoa mwito wa kufanyika kwa juhudi za pamoja kutoa huduma za afya kwa watu waliokimbia makazi yao wanaoishi na VVU nchini Ethiopia.

Katika taarifa yake iliyotolewa Jumatatu Desemba Mosi kwenye maadhimisho ya siku ya kupambana na UKIMWI Duniani, shirika hilo limesema Ethiopia inakabiliwa na janga la pande tatu za mgogoro wa ndani, mabadiliko ya tabianchi, na suala la wakimbizi, ambalo linazuia uwezo wa kutoa huduma muhimu za afya na usaidizia mwingine wa kibinadamu kwa watu walio hatarini, ikiwa ni pamoja na wale wanaoishi na VVU.

UNAIDS imesema kwenye misukosuko ya kibinadamu, huduma muhimu kwa watu wenye VVU na afya ya uzazi huwekwa pembeni ikilinganishwa na mahitaji ya dharura ya chakula, makazi na udhibiti wa magonjwa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha