

Lugha Nyingine
Waziri wa ulinzi wa Sudan asema Jeshi la Sudan limedhibiti tena maeneo muhimu ya katikati ya nchi
Waziri wa ulinzi wa Sudan Yassin Ibrahim Yassin amesema Jeshi la Sudan (SAF) limedhibiti tena maeneo muhimu ya katikati ya nchi hiyo wakati ambapo mapigano na askari wa Vikosi vya Mwitikio wa Haraka (RSF) yakiendelea katika mji mkuu Khartoum.
Waziri huyo amesema Jeshi la Sudan limekomboa eneo la Umm Al-Qura karibu na Wad Madani katika Jimbo la Gezira, na pia limedhibiti tena eneo la Kiwanda cha Sukari cha Sinnar na kufika eneo la vitongoji vya Umm Ruwaba katika Jimbo la Kordofan Kaskazini.
Kwa mujibu wa shuhuda mmoja mjini Khartoum, mapigano makali kati ya SAF na RSF yalitokea alfajiri ya Jumatatu katika makazi ya Shambat katika mji wa Bahri.
Katika siku kadhaa zilizopita, Jeshi la Sudan lilitangaza kutekeleza operesheni nyingi na kuangamiza kambi za RSF katika eneo la Bahri.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma