Ghana yafanya upigaji kura maalum kabla ya uchaguzi mkuu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 03, 2024

Mpiga kura akipiga kura kwenye upigaji kura maalum mjini Accra, Ghana, Desemba 2, 2024. (Picha na Seth/Xinhua)

Mpiga kura akipiga kura kwenye upigaji kura maalum mjini Accra, Ghana, Desemba 2, 2024. (Picha na Seth/Xinhua)

ACCRA – Mapema jana Jumatatu vituo vya upigaji kura vilivyowekwa kwenye sehemu mbalimbali nchini Ghana vimefunguliwa kwa ajili ya upigaji kura maalum kabla ya uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Desemba 7, ambapo upigaji kura huo maalum unawezesha watu binafsi, wakiwemo walinzi wa usalama, waandishi wa habari, maofisa wa tume ya uchaguzi na wanaharakati wa mashirika ya kiraia wapige kura zao mapema, kwani watu hao watakuwa wakitekeleza majukumu yao mbali na vituo vya kupigia kura wakati wa uchaguzi mkuu.

Tume ya Uchaguzi ya Ghana (EC) imesema watu takriban 131,478, wanaochukua asilimia 0.007 ya wapiga kura wote waliojiandikisha, wana haki ya kupiga kura zao katika upigaji kura maalum wa Jumatatu.

Zanetor Agyeman-Rawlings, mbunge aliyeko madarakani sasa wa Jimbo la Korle-Klottey, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kuwa mchakato huo wa upigaji kura maalum ulikuwa ukiendelea vizuri asubuhi nzima ya siku hiyo.

"Upigaji kura ulianza kwa wakati, ambapo idadi kubwa ya watu wamekuja kupiga kura zao. Hakujawa na hitilafu zozote," Agyeman-Rawlings amesema. "Kama kile tunachokiona leo kitajirudia Desemba 7, watu watakuwa na mwelekeo wa kukubali matokeo. Ili hilo litokee, EC lazima ibebe wajibu wake wa kuwa mwamuzi asiyependelea upande wowote."

Kwa mujibu wa EC, upigaji kura maalum wa Mikoa ya Magharibi na Mashariki umeahirishwa hadi Desemba 5 kutokana na kuonekana hadharani kwa baadhi ya karatasi za kupigia kura kabla ya wakati.

Desemba 7, wapiga kura kote nchini Ghana watapiga kura kumchagua rais na wabunge wapya 276. 

Mpiga kura akipiga kura kwenye upigaji kura maalum mjini Accra, Ghana, Desemba 2, 2024. (Picha na Seth/Xinhua)

Mpiga kura akipiga kura kwenye upigaji kura maalum mjini Accra, Ghana, Desemba 2, 2024. (Picha na Seth/Xinhua)

Watu wakijiandikisha kwenye kituo cha kupiga kura  wakati wa upigaji kura maalum mjini Accra, Ghana, Desemba 2, 2024. (Picha na Seth/Xinhua)

Watu wakijiandikisha kwenye kituo cha kupiga kura wakati wa upigaji kura maalum mjini Accra, Ghana, Desemba 2, 2024. (Picha na Seth/Xinhua)

Mpiga kura akipiga kura wakati wa upigaji kura maalum mjini Accra, Ghana, Desemba 2, 2024. (Picha na Seth/Xinhua)

Mpiga kura akipiga kura wakati wa upigaji kura maalum mjini Accra, Ghana, Desemba 2, 2024. (Picha na Seth/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha