

Lugha Nyingine
Rais wa Jamhuri ya Korea atangaza sheria ya utawala wa kijeshi wa dharura, ambayo imeondolewa saa chache katika mkutano wa baraza la mawaziri
Picha hii iliyopigwa katika Stesheni ya Seoul mjini Seoul, Jamhuri ya Korea, Desemba 3, 2024 ikionyesha skrini inayomuonyesha Rais wa Jamhuri ya Korea Yoon Suk-yeol akitangaza sheria ya utawala wa kijeshi wa dharura katika hotuba ya moja kwa moja kwenye televisheni. (Xinhua/Yao Qilin)
SEOUL - Rais wa Korea Kusini Yoon Suk-yeol Yoon alitangaza sheria ya utawala wa kijeshi wa dharura jana Jumanne usiku, ikiwa ni amri ya kwanza ya kutekeleza sheria ya utawala wa kijeshi tangu udikteta wa kijeshi wa nchi hiyo kumalizika mwishoni mwa miaka ya 1980, hata hivyo, sheria hiyo aliyoitangaza rais huyo imeondolewa mapema leo Jumatano kwenye mkutano wa baraza la mawaziri baada ya Bunge la taifa la nchi hiyo kupiga kura kuipinga.
Pendekezo la kuondoa amri ya hiyo ya kutekeleza sheria ya utawala wa kijeshi imeidhinishwa kwenye mkutano wa baraza la mawaziri ulioitishwa kwa dharura, vyombo vingi vya habari vimeripoti.
Kabla ya mkutano huo, Yoon alisema katika hotuba yake kwa njia ya televisheni kwamba askari watekelezaji wa sheria hiyo ya utawala wa kijeshi walikuwa wameondolewa wakati Bunge la Taifa likitaka sheria hiyo kuondolewa, akiapa kuondoa sheria hiyo ya utawala wa kijeshi kwenye mkutano wa baraza la mawaziri ili kukubali matakwa ya bunge.
Rais amelitaka Bunge kuacha kudumaza mambo ya nchi kwa kujaribu kuwapigia kura ya kutokuwa na imani na kuwaondoa madarakani viongozi wa serikali, kupunguza bajeti ya serikali ya mwaka ujao na kuanzisha kikundi maalum cha maofisa wa uendeshaji mashtaka kufanya uchunguzi juu ya kashfa ya mke wa rais.
Bunge la taifa liliitisha mkutano wa wajumbe wote, likipitisha azimio la kuondoa sheria hiyo ya utawala wa kijeshi, ambapo wabunge 18 wa chama tawala cha People Power na wabunge 172 wa vyama vya upinzani wamehudhuria mkutano huo na kupiga kura ya ndiyo.
Kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo, rais anapaswa kuondoa sheria ya utawala wa kijeshi wakati bunge lenye wabunge 300 likitaka kuondoa sheria hiyo huku wabunge wengi wakipiga kura ya ndiyo.
Awali akitangaza sheria hiyo, Yoon alisema kwamba "Ninatangaza sheria ya utawala wa kijeshi wa dharura" ili kutokomeza nguvu zinazopinga nchi na kushikilia utaratibu huru wa katiba.
Alibainisha kuwa ni hatua isiyoepukika kuhakikisha uhuru wa watu, usalama na uendelevu wa nchi kuepusha nguvu za kupinga nchi zinazotaka kupindua nchi, akiapa kuondoa nguvu hizo za kupinga nchi na kurejesha hali ya kawaida ya nchi haraka iwezekanavyo.
Watu wakisubiri katika foleni kwenye kituo cha usafiri wa umma nje ya stesheni ya reli mjini Seoul, Jamhuri ya Korea, Des. 3, 2024. (Xinhua/Yao Qilin)
Polisi na magari ya dharura yakionekana kazini kwenye barabara nje ya ofisi ya rais mjini Seoul, Jamhuri ya Korea, Des. 4, 2024. (Xinhua/Yao Qilin)
Polisi wakionekana kazini nje ya ofisi ya rais mjini Seoul, Jamhuri ya Korea, Des. 4, 2024. (Xinhua/Yao Qilin)
Polisi wakionekana kazini nje ya ofisi ya rais mjini Seoul, Jamhuri ya Korea, Des. 4, 2024. (Xinhua/Yao Qilin)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma