Namibia yachagua rais wa kwanza mwanamke

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 04, 2024

Picha iliyopigwa Novemba 27, 2024 ikimuonyesha Netumbo Nandi-Ndaitwah (katikati) akihojiwa nje ya kituo cha kupigia kura mjini Windhoek, Namibia. (Picha na Ndalimpinga Iita/Xinhua)

Picha iliyopigwa Novemba 27, 2024 ikimuonyesha Netumbo Nandi-Ndaitwah (katikati) akihojiwa nje ya kituo cha kupigia kura mjini Windhoek, Namibia. (Picha na Ndalimpinga Iita/Xinhua)

WINDHOEK - Namibia imeweka historia siku ya Jumanne kwa kumchagua rais wa kwanza mwanamke wa nchi hiyo, Netumbo Nandi-Ndaitwah mwenye umri wa miaka 72 kutoka chama tawala cha South West Africa People's Organisation (SWAPO) ambapo ni tukio muhimu katika uchaguzi wa rais na wabunge wa Namibia Mwaka 2024.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Namibia (ECN) Elsie Nghikembua alitangaza ushindi huo mkubwa Jumanne jioni, akitambua kilele cha mchakato wa kipindi cha uchaguzi ulioanza Novemba 27.

Hata hivyo, kutokana na kutatizwa kwa siku ya kwanza ya upigaji kura, mchakato huo uliongezwa muda katika baadhi ya maeneo kuanzia Novemba 29 au 30 ili kuhakikisha kwamba wapigakura wote wenye haki ya kupiga kura wanapata fursa ya kushiriki.

Wananchi walijitokeza kwa wingi kushiriki katika uchaguzi huo uliokuwa na matarajio makubwa, huku ECN ikisema kuwa wapiga kura karibu milioni 1.45 wenye haki ya kupiga kura waliandikishwa, huku kura za urais zikiwa ni 1,099,582 na kura za Bunge la Taifa 1,092,685.

Nandi-Ndaitwah, ambaye amekuwa rais wa tano tangu nchi hiyo kupata uhuru mwaka 1990, ameshinda kwa asilimia 57.31 ya kura, na amefuatiwa na mpinzani wake wa karibu Panduleni Itula wa chama cha Independent Patriots for Change ambaye amepata asilimia 25.50.

Katika hotuba yake ya kukubali ushindi, Nandi-Ndaitwah amesema ana furaha kuweza "kulipatia taifa mwongozo kuhusu ajenda yetu ya maendeleo na uimarishaji wa utaratibu wetu."

“Pia ninapenda kuwashukuru wale ambao wameonyesha upendo wao kwa nchi kwa kuhakikisha kwamba amani na utulivu vinaendelea kukua, hasa katika mchakato wa uchaguzi wetu,” ameongeza.

Wakati huo huo, kuna wajumbe 104 katika Bunge la Taifa la Namibia, kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo.

Katika uchaguzi wa Bunge uliofanyika sambamba na ule wa urais, Chama cha SWAPO cha Rais huyo Mteule Nandi-Ndaitwah kilipata viti 51, huku Panduleni Itula wa chama cha Independent Patriots for Change akipata viti 20.

SWAPO kimekuwa chama tawala nchini Namibia tangu nchi hiyo ilipopata uhuru mwaka 1990.

Picha iliyopigwa Novemba 27, 2024 ikimuonyesha Netumbo Nandi-Ndaitwah (katikati) akihojiwa nje ya kituo cha kupigia kura mjini Windhoek, Namibia. (Picha na Ndalimpinga Iita/Xinhua)

Picha iliyopigwa Novemba 27, 2024 ikimuonyesha Netumbo Nandi-Ndaitwah (katikati) akihojiwa nje ya kituo cha kupigia kura mjini Windhoek, Namibia. (Picha na Ndalimpinga Iita/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha