

Lugha Nyingine
Tiba ya Jadi ya Kichina yapata umaarufu Zimbabwe
(CRI Online) Desemba 04, 2024
Tiba ya Jadi ya Kichina (TCM) inapata umaarufu nchini Zimbabwe kufuatia kufunguliwa kwa chumba cha maonesho ya TCM katika Kituo cha TCM na Akyupancha cha Zimbabwe-China, kilichoko katika Kundi la Parirenyatwa la Hospitali mjini Harare.
Chumba hicho cha maonesho, kilichofunguliwa mwezi Juni, kinalenga kuonesha utamaduni wa Tiba ya Jadi ya Kichina na matumizi yake kwa umma.
Mkurugenzi wa kituo hicho, Hu Sha amesema anatumai kuwa chumba hicho cha maonesho kitakuwa jukwaa na dirisha kwa wenyeji kufahamu TCM na kuhimiza ushirikiano kati ya TCM na tiba ya jadi ya Zimbabwe.
Idadi ya wagonjwa wanaopokea matibabu bila malipo katika Kituo cha TCM na Akyupancha imeongezeka kwa kiasi kikubwa tangu kituo hicho kilipofunguliwa kwa umma mwaka 2020.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma