Madaktari wa China waleta ahueni kwa watu wa Sudan Kusini

(CRI Online) Desemba 04, 2024

Kundi la 12 la Timu ya Madaktari wa China nchini Sudan Kusini limetibu mamia ya wagonjwa huko Lobonok Payam Kusini mwa Juba ikiwa ni mara ya pili kwa kundi hilo la madaktari wa China kwenda kutoa huduma katika eneo hilo baada ya ziara ya mwisho ya kundi la 11, ambalo liliondoka mapema mwaka huu.

Baadhi ya wanafunzi ni moja ya makundi ya watu walionufaika na huduma za matibabu bila malipo, kwenye kambi ya matibabu iliyowekwa na kundi hilo katika Kijiji cha Yapa siku ya Jumatatu.

Madaktari hao pia waliwaelekeza baadhi ya wagonjwa waliokuwa na hali mbaya kwenda kwa matibabu zaidi kwenye hospitali ya rufaa ya mafunzo ya Juba, ambayo ndiyo makao yao makuu.

Serikali ya China ilituma kundi la kwanza la madaktari wa China nchini Sudan Kusini mwaka 2012, hadi sasa makundi ya madaktari wa China yametoa mchango mkubwa katika kuboresha huduma za Afya nchini Sudan Kusini.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha